25.2 C
Dar es Salaam
Sunday, August 14, 2022

Papa Francis: Wanawake wana madai halali kutaka haki zaidi

VATICAN CITY, VATICAN

KIONGOZI wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis, amesema wanawake wana madai halali ya kutaka usawa katika kanisa, lakini alisita kuidhinisha miito ya moja kwa moja kutoka kwa maaskofu wake juu ya umuhimu wa mabadiliko makubwa.

Papa Francis alisema hayo katika waraka wake mrefu unaoitwa ‘Yesu bado yuko hai’ lakini hakuidhinisha hitimisho kama  hilo.

Alisema kanisa linalowasikiliza vijana linapaswa pia kuyazingatia madai halali ya wanawake juu ya haki na usawa.

Ameeleza kuwa kanisa lina jukumu la kutoa mafunzo mazuri zaidi kwa wanaume na wanawake wenye uwezo wa kuongoza.

Waraka uliotolewa na Papa Francis, kwa ajili ya vijana Wakatoliki wa leo, unatokana na mkutano wa maaskofu uliofanyika Oktoba mwaka jana.

Katika mkutano huo, maaskofu walijadili njia bora ya kuwahudumia vijana huku suala la utashi wa haki zaidi kwa wanawake likiwa pia kipaumbele.

Katika azimio lao, maaskofu walitoa wito kutaka wanawake wapewe nafasi za uongozi na mamlaka ya kushiriki katika kupitisha maamuzi ya kanisa.

Katika hati yake, Papa Francis alisema kanisa linapaswa kuiangalia historia yake na kutambua kwamba pamekuwepo udikteta wa wanaume, utumwa wa aina mbalimbali na unyanyasi wa kingono.

Kutokana na mwenendo huo, alisema anaweza kuunga mkono miito juu ya kuheshimu zaidi haki za wanawake na pia kuunga mkono usawa baina ya wanawake na wanaume licha ya kutokubaliana na hoja zote zilizotolewa na watetezi wa haki za akina mama.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,695FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles