24.8 C
Dar es Salaam
Friday, October 4, 2024

Contact us: [email protected]

Papa Francis atangaza vita kashfa ya udhalilishaji watoto

VATICAN CITY, Vatican

KIONGOZI Mkuu wa Kanisa Katoliki ulimwenguni, Papa Francis, ameahidi kuchukua hatua kali ili kukomesha vitendo vya udhalilishaji kijinsia kwa watoto kufuatia kashfa inayowaandama baadhi ya viongozi wa Kanisa hilo.

Kiongozi huyo Mkuu alitoa ahadi hiyo wakati akifunga Mkutano Mkuu wa Kanisa Katoliki, uliomalizika jana mjini Vatican.

Katika hotuba huyo, kiongozi huyo alisema watumishi wa Kanisa hilo ambao wanakabiliwa na kashfa hiyo ya udhalilishaji watoto kijinsia ni watumishi wa shetani na huku akiahidi kukabiliana na kila kesi kwa uzito mkubwa.

Alisema unyanyasaji wa kijinsia kwa watoto anamkumbusha kuhusu ibada za kuwatoa watoto kafara katika ibada za kipagani.

“Vitendo hivi vinanikumbusha kuhusu mazoea ya kikatili katika dini za kipagani  au kuenea kwa tamaduni fulani,” alisema kiongozi huyo.

Kauli hiyo Papa Francis imekuja wakati katika kipindi cha wiki ijayo, Vatican ikijiandaa kutoa mwongozo wa  kushughulikia mashtaka ya unyanyasaji  kisheria kulingana na mapendekezo yaliyotolewa katika mkutano huo.

Akizungumzia mwongozo huo, kiongozi huyo alisema kuwa, kwa sasa waathirika watapewa kipaumbele na kwamba itatolewa miongozo mingine mipya iliyo wazi ambayo itawahimiza kuchukua hatua.

Baba huyo Mtakatifu vilevile aliahidi kukomesha mambo ya kuficha na akasema kuwa, wote wakaohusika na  vitendo vya aina hiyo watafikishwa mbele ya sheria.

“Hakutakuwapo na simile katika vitendo hivi vya udhalilishaji watoto kijinsia,” alisema kiongozi huyo mkuu.

“Hiki ni kilio cha kimya kimya cha watoto wadogo ambao badala ya kutafuta baba na miongozo ya kiroho wanakutana na watesaji,” aliongeza kiongozi huyo.

“Ni wajibu wetu kulipa kilio hiki cha kimya kilichochochewa,” aliongeza zaidi Baba Mtakatifu huyo.

Wakati kiongozi huyo anachaguliwa mwaka  2013, alitakiwa kuchukua hatua kali kuhusu janga hilo, lakini wakosoaji wanasema kuwa hajachukua hatua za kutosha kuwashughulia maaskofu ambao wanatuhumiwa kuhusika na vitendo hivyo.

Wakosoaji hao wanasema kwamba maelfu ya watu duniani kote wamekuwa wakilalamika kudhalilishwa kijinsia na  baadhi ya viongozi hao wa dini kwa miongo kadhaa, lakini Kanisa hilo Katoliki limekuwa likizificha shutuma hizo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles