30.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Papa Francis amtangaza kadinari Newman mtakatifu mpya

ROME, ITALIA

BABA Mtakatifu, Papa Francis amemtangaza Kadinali John Henry Newman kuwa Mtakatifu wa Kanisa Katoliki, katika maadhimisho ya misa iliyofanyika jana  huko Rome, Italia.

Papa Francis alimyangaza Newman kuwa Matakatifu katika Misa ya wazi iliyohudhuriwa na maelfu ya watu waliokwenda kwenye hija mjini humo.

Kadinali Newman, ambaye alifariki huko Birmingham mwaka 1890, ni muingereza wa kwanza kutangazwa kuwa mtakatifu kwa kipindi cha takribani miaka 50.

Mwana mfalme Wales, Prince Charles alijumuika katika misa hiyo ambayo ilikuwa inawatambua wanawake wengine wanne kuwa watakatifu.

Mama Mariam Thresia kutoka India, Marguerite Bays kutoka Uswizi, Mama Giuseppina Vannini kutoka Italia na sista aliyezaliwa Brazili, Dulce Lopes Pontes walikuwa wanatambuliwa pia kuwa watakatifu katika misa hiyo.

Mtakatifu John Henry Newman ni muingereza wa kwanza kutambulishwa tangu mwaka 1970

Maelfu ya waingereza walisafiri mpaka Rome ili kusheherekea utambulisho huo.

Carol Parkinson, Katibu wa marafiki wa Newman kutoka mji wa Birmingham, alisema kuwa kutangazwa kwa mtakatifu huyo ni kwa kipekee na imekuwa siku ya hisia kubwa kwao.

“Uadilifu wake, urafiki wake, uaminifu pamoja na bidii aliyoweka katika kazi yake ni mfano mzuri wa kuigwa na kila mtu,” alisema.

Kadinali Newman alizaliwa mjini London mwaka 1801, alisoma chuo cha Trinity College na Oxford.

Alikuwa anatarajiwa kuwa padri wa kianglikana lakini alibadili dini na kuwa mkatoliki mwaka 1845.

Newman alisifika kwa miujiza miwili, muujiza wa kwanza ni kumponya mgonjwa wa uti wa mgongo wa kiume na kumponya mwanamke aliyekuwa haachi kutokwa damu.

BBC

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles