26.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 6, 2023

Contact us: [email protected]

PAPA FRANCIS AKIRI YUKO HATARINI KUSHAMBULIWA

VATICAN CITY, VATICAN


pope_francisKIONGOZI Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis, anasema anatambua kwamba anaweza kuwa mlengwa wa shambulio la kigaidi, lakini ataendelea na ziara zake bila ya kutumia mavazi na magari ya kiusalama yenye kuzuia risasi kwa sababu anataka kuwa karibu na watu.

Hii ni kwa mujibu wa maelezo katika utangulizi wa kitabu chake kipya, ambacho kimeandikwa na mwandishi wa Italia Andrea Tornielli.

Tofauti na watangulizi wake waliotumia mavazi na magari ya kiusalama, Papa Francis hutumia mavazi na magari ya kawaida katika ziara zake nje.

Kitabu hicho kiitwacho ‘Kusafiri’, kinahusu ziara 17 ambazo Papa Francis amefanya katika nchi zaidi ya 25 tangu achukue wadhifa huo mwaka 2013.

Francis amesema anafahamu hatari zilizopo, lakini hana woga kumhusu bali kwa wanaosafiri naye na zaidi wale anaokutana nao katika nchi mbalimbali.

‘Daima kuna hatari kutoka kwa kichaa, lakini Bwana daima yupo kwa ajili yetu.”

Papa, anatarajia kufanya safari mbili za kimataifa mwaka huu, moja nchini Ureno, nyingine India na Bangladesh.

Alisema: “Nafahamu fika hitaji la usalama na ninashukuru wanausalama, lakini askofu ni mchungaji, baba, hivyo hapaswi kuwa na vikwazo vingi baina yake na watu.”

‘Kwa sababu hii nilishaweka wazi tangu mwanzo kuwa nitakuwa tayari kusafiri pale tu nitakapoweza kuonana na watu.”

Kwa kipindi cha miaka miwili iliyopita, polisi wa Italia wameongeza ulinzi eneo kuzunguka Vatican, taifa huru lililopo katikati ya Rome, kufuatia mashambulizi yanayofanywa na wanamgambo wenye itikadi kali Ulaya.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles