31.7 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Papa amemteua Nyaisango kuwa Askofu Mkuu Jimbo la Mbeya

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

PAPA Francisko amemteua Askofu Gervas Nyaisango kuwa Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Mbeya, litakalokuwa na majimbo ya Iringa na Sumbawanga.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari Dar es Salaam jana na Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC), Padre Charles Kitima, ilieleza kuwa uteuzi huo ni baada ya Papa kulipandisha hadhi Jimbo la Mbeya na kuwa jimbo kuu.

Taarifa hiyo ilieleza kuwa kabla ya uteuzi wa Askofu Nyaisango atakayekuwa wa kwanza kuongoza jimbo hilo, alikuwa Rais TEC na Askofu wa Jimbo la Mpanda, Tabora.

Takwimu za kanisa za mwaka huu  zinaonyesha kuwa Jimbo Kuu la Mbeya linaundwa na Parokia 48 zinazohudumiwa na mapadre 73 wa jimbo, mapadre watawa 15, watawa wa kiume 15 na watawa wa kike 299.

WASIFU WAKE

Askofu Nyaisonga alizaliwa Novemba 3, 1966 huko Bunda mkoani Mara. Baada ya masomo yake ya msingi na sekondari huko Mbeya na Sumbawanga, mwaka 1989 alijiunga na Seminari Kuu ya Kibosho, Moshi kwa ajili ya masomo ya falsafa.

Kisha aliendelea na masomo ya Kitaalimungu Segerea, Jimbo Kuu la Dar es Salaam ambako alihitimu na kuwekewa mikono kama shemasi mwaka 1995 alioufanya katika Parokia ya Itaka, Jimbo Katoliki la Mbeya.

Julai 11, 1996 alipewa daraja Takatifu ya Upadre Jimbo Katoliki la Mbeya, akiwekewa mkono na Askofu Yakobo Dominic Sangu. Baada ya Upadrisho alifanya utume katika sehemu mbalimbali za Jimbo Katoliki Mbeya kama Paroko wa Usu na Mwalimu wa Seminari Ndogo ya Mbalizi.

Kuanzia mwaka 1998 hadi 2001, alijiendeleza na masomo ya juu katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) ambako alipata shahada ya kwanza na kurudi kuendelea na kazi kama Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Pandahill kuanzia mwaka 2001 hadi 2006.

Aliendelea na masomo ya elimu ya juu (UDSM) mwaka 2006 hadi 2009, akijipatia Shahada ya Uzamili katika masomo ya Sayansi Jamii na kuanzia mwaka huo hadi 2011, alikuwa Mhadhiri Msaidizi katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino cha Tanzania (SAUT).

Agosti, 2010 alitumwa nchini Ujerumani kusoma masomo ya juu zaidi kama sehemu ya maandalizi ya kuwa mwalimu katika somo la jiografia ambapo kabla ya kuhitimu masomo yake Januari 9, 2011, akapokea simu kutoka kwa Balozi wa Vatican nchini Tanzania ikimtaarifu kuwa ameteuliwa na Baba Mtakatifu Mstaafu, Benedikto XVI, kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki Dodoma.

Februari 2, 2014 aliteuliwa na Baba Mtakatifu Francisko kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Mpanda na kusimikwa  Mei 4, 2014 akihudumu huko hadi alipoteuliwa kuwa Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Mbeya jana.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles