29.2 C
Dar es Salaam
Monday, October 3, 2022

PANYA MMOJA HUTUMIA MILIONI 2.5 KUTAMBUA MAAMBUKIZI YA TB

Veronica Romwald, Dar es Salaam

Panya buku mmoja anayetumika kutambua sampuli za wagonjwa wenye maambukizi ya Kifua Kikuu (TB), hutumia Sh milioni 2.5 ili kumkuza na kupatiwa mafunzo maalumu ya kutambua ugonjwa huo.

Hayo yamesemwa na Mtafiti wa Kituo cha Udhibiti wa Viumbe Hai waharibifu wa Chuo Kikuu cha Sokoine (SUA-APOPO), Dk. Georges Mgode, wakati akizungumza na waandishi wa habari wakati wa Kongamano la Kwanza la watafiti waliojikita kuchunguza ugonjwa wa kifua kikuu na ukoma lililoandaliwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.

“Ingawa ni panya buku lakini wale si wa majumbani, huwa tunakwenda kuwakamata wazazi wao huko porini, tunawalea, wanapozaana tunawachukua wale watoto na kuanza kuwapa mafunzo maalumu kwa kutumia mtaala tulioandaa,” amesema.

Amesema wapo panya ambao huchukua miezi sita kuelewa mafunzo na wengine hadi miezi tisa na huweza kufanya kazi hadi anapofikisha miaka saba hadi nane.

“Hivyo tunatumia kiasi cha Dola 1,000 ambayo ni sawa na Sh milioni 2.5 kumkuza panya mmoja, hiyo inahusisha chakula na dawa.

“Kwa mujibu wa utafiti wa Shirika la Afya Duniani (WHO), mwaka 2016 inakadiriwa kuwa na wagonjwa 160,000 wapya wa TB kwa mwaka lakini uwezo wa kuwatambua ni wagonjwa 65,500 sawa na asilimia 41,” amesema.

Pamoja na mambo mengine, amesema kuna wagonjwa 96,000 ambao hawagunduliwi na hiyo ni changamoto kwani wengi hawaendi hospitalini na wapo ambao huenda kwa waganga wa kienyeji, lakini wale wanaokuja asilimia 90 hupona kabisa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,587FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles