28.6 C
Dar es Salaam
Friday, January 28, 2022

PAMPU MONEY MAKER HUONGEZA WINGI WA MAZAO

Na Joseph Lino


ASILIMIA 80 ya wakulima wadogo Afrika wana ukosefu wa fursa za kilimo ambapo huangukia katika umasikini wa kutupwa.

Wakulima hao wanategemea kilimo cha mvua ambacho huvuna mara moja kwa mwaka, hivyo hufanya familia zao kukumbwa na balaa la njaa na umasikini. 

Kutokana na hali ya ukame ambayo inasababisha mabadiliko ya tabia nchi, mvua hainyeshi kama ilivyokuwa miaka ya nyuma na hawana njia mbadala ya kuweza kuzalisha chakula.

Hata hivyo, kuna njia za kuwawezesha wakulima wadogo katika kilimo cha umwagiliaji kwa kutumia teknolojia ya pampu za umwagiliaji ambazo hazitumii umeme au mafuta.

Taasisi ya Kick Start International kwa muda mrefu  imekuwa ikisambaza pampu za kisasa ambazo zinamwezesha mkulima kufanya shughuli za kilimo bila kikomo mwaka mzima.

Pampu za umwagiliaji ambazo hujulikana kama ‘Money Maker’ zilitengenezwa kwa lengo la kusaidia wakulima kukabiliana na ukame ili kurejesha mavuno na kuwafanya wawe imara zaidi kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Kwa mujibu wa Kick Start, pampu za Money Maker ambayo ilibuniwa kwa ili kuwapatia wakulima kwa gharama nafuu kutokana kwamba wengi wao ni masikini na wana mahitaji ya muhimu ya haraka ambalo hitaji kubwa ni kutengeneza pesa.

Meneja wa Thamini na Uangalizi wa Kick Start, Mwaluko Mpangwa, anasema wakulima masikini huishi katika ulimwengu wa uchumi wa pesa taslimu na wanataka pesa ya mahitaji yao muhimu kama ada na matibabu.

Anaelezea kuwa Pump za Money maker zinamwezesha mkulima kuzalisha pesa kwa mwaka mzima kupitia umwagiliaji hasa kipindi ambacho bei ya mazao ipo juu.

Mpangwa anasema mvua ni muhimu lakini watu waondokane  na akili za kutegemea mvua tu na hivyo kuingia katika kilimo cha umwagiliaji.

 “Mvua siku hizi imekuwa si tegemezi  tena, ila kama wakulima wanaweza kutumia pampu hasa kwa wakulima masikini, wana uwezo wa  kuzalisha chakula mwaka nzima na kupata faida na kuondokana na umasikini wa kutupwa,” anasema Mpangwa.

Mtaalamu huyo wa kilimo anaelezea kuwa kilimo cha umwagiliaji kinawezesha mazao kuhimili na kustawi kipindi ambacho kuna upungufu wa mvua na kinatoa nafasi kubwa ya kuiwezesha Tanzania kujitosheleza kwa chakula na kupatikana kwa chakula cha ziada cha kuuza nje ya nchi.

Aidha, inaelezwa kwamba kilimo cha umwagiliaji  kama kitaendelezwa zaidi kutokana na nchi yetu kuwa maji mengi katika mito, maziwa, mabonde, malambo na hata maji yanayopatikana chini ya ardhi sambamba na maeneo lukuki yanayofaa kwa kilimo, Tanzania ina nafasi kubwa ya kuwa ghala la chakula la Afrika.

Kwa upande wa Taasisi ya Kick Start hushirikiana na wadau wengine katika kuelimisha, kutoa mafunzo ya kilimo cha umwagiliaji na pampu ili kufikia malengo. 

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
177,065FollowersFollow
532,000SubscribersSubscribe

Latest Articles