24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Pamba nyingine tani 20 yataifishwa Bariadi

Derick Milton, Simiyu

Zikiwa zimepita siku kumi tangu Mkuu wa Wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu Festo Kiswaga, ataifishe tani 26 za pamba iliyodaiwa kununuliwa kwa njia ya machinga, leo Jumamosi Agosti 24, Mkuu huyo wa Wilaya ametaifisha pamba nyingine tani 20.

Akiongea na waandishi wa habari Kiswaga amesema kuwa pamba hiyo imekamatwa katika kijiji cha Igegu kata ya Sapiwi majira ya saa 5 asubuhi ikiwa imepakiwa kwenye gari aina ya scania yenye namba za usajili T 729 ARN.

Amesema kuwa kupitia kikosi kazi ambacho alikiunda cha kupambana na watu wanaonunua pamba kwa njia ya machinga, gari hilo baada ya kukamatwa dereva aliweza kukimbia kusikojulikana.

“Kikosi kazi hiki baada ya kukamata, kilikuta pamba haina kibali chochote na haikujulikani wapi inaenda, nani mmliki wake, na hata gari halijajulikana ni mali ya nani,” amesema Kiswaga.

Amesema kuwa ilibainika kuwa pamba hiyo ilikuwa inanunuliwa kwa njia za machinga, ambapo wakulima walikuwa wakinunuliwa kwa sh.600 hadi 800 kutoka katika kijiji hicho.

“Baada ya kubaini hivyo nimeamua kuitaifisha pamba hii na tutaenda kuiuza leo kwenye kiwanda cha kuchambua pamba chochote na pesa yote ambayo itapatika tutaipeleka katika kukamilisha ujenzi wa vyumba vya madarasa shule ya msingi Igegu,” amesema Kiswaga.

Aidha amewaonya viongozi wa Vyama vya Msingi vya Ushirika (Amcos) ambao wamekuwa wakishirikiana na makampuni kununua pamba kwa njia ya umachinga kuwa watakamatwa na kuchukuliwa hatua.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles