25.1 C
Dar es Salaam
Saturday, December 9, 2023

Contact us: [email protected]

Pacha wa Kagera watenganishwa kwa Sh bilioni 1.1

AVELINE KITOMARY-DAR ES SALAAM

PACHA  waliougana Anisia na Melnes Bernard,  wamewasili jana katika uwanja wa ndege wa Julius  Nyerere jijini Dar es salaam  wakitokea nchini  Saudi Arabia baada ya kutenganishwa, matibabu yaliyogharimu dola za Marekani 500,000 (zaidi ya Sh bilioni 1.1)

Mapacha hao walikuwa wameungana kifua, tumbo na nyonga walianza kufanyiwa upasuaji wa kutenganishwa Disemba 23 katika hospitali ya King Abdallah.

Baada ya kutenganishwa, pacha hao ambao walizaliwa wakiwa na miguu mitatu, sasa kila mmoja amebaki na mmguu mmoja.

Wakizungumza wakati walipowasili, madaktari bingwa wa upasuaji kwa watoto walisema waliungana na madaktari 35 wa Saudi Arabia na nchi zingine  ili kufanikisha upasuaji huo ambao ulifanyika ndani ya sasa 14.

Mmoja wa Madaktari hao Dk Petronia Ngiroi, alisema madktari bingwa wa sehemu mbalimbali wa watoto walifanya uchunguzi na kuhakikisha kuwa upasuaji huo utafanikiwa.

“Tangu wakiwa Muhimbili tuliwafanyia vipimo na tukawasiliana na madktari wa Saudi Arabia na tukawatumia vipimo wakatuambia inawezekana kufanyiwa upasuaji baada ya hapo tukaanza safari Julai 8 mwaka jana.

“Tuliposafiri tulipokelewa vizuri na watoto wakaanza kupatiwa vipimo mbalimbali kwani umbali wa kutoka huku mpaka kule uliwafanya wawe na infection hivyo wakawafanyia consultation kwa madaktari wa mifupa, kibofu cha mkojo, madktari wa upasuaji kwahiyo wataalamu karibia wote waliwaona watoto,”alieleza Dk Ngiroi.

 Daktari mwingine Dk Zainab Bohari, alisema pamoja na kuwa watoto hao waliungana, kila mmoja anaweza kuwa na tabia yake na wanauwezo wa kuishi muda mrefu kama watu wengine .

“Kutenganishwa kwa kutawapa uhuru kwani tulipenda wote wawili watoke salama, walikuwa na miguu mitatu lakini kila mmoja amerudi na mguu mmoja na mguu wa tatu ulitumika kuziba vidonda vya upasuaji.

“Hawa watoto wamenufaika kupitia ushirikiano  mzuri na Saudi Arabia, tukumbuke watoto hawa walitokea Bukoba hivyo tutafatilia hali zao mpaka wawe watu wazima hasa afya zao,”alisema Dk Bohari.

Kwa upande wake Naibu  Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto, Dk Elias  Kwesi, alisema anashukuru ubalozi wa Saudi Arabia kwa ushirikiano waliouonesha  hadi kuwarudisha watoto hao kuwa salama.

Naye Katibu Mkuu wa Waizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mwinyi, alisema Serikali ya Tanzania inashirikiana kikamilifu na Serikali ya Saudi Arabia ambapo walitoa mashine na vifaa tiba 64.

“Walitupa mashine na vifaa ambavyo viligawavywa bara walipata mashine 45 na Zanzibar walipewa 17 na pia msaada huu ambao tumepata kwa watoto hawa ni mkubwa pia,”alisema Mwinyi.

Kwa upande wake mama wa watoto hao, Jonensia Jovitus, aliwashukuru watu wote walioshiriki katika kufanikisha matibabu ya watoto wake.

“Napenda kuwashukuru wote kwani tokea ninamimba ya hawa watoto nilipata shida sana lakini kwa uwezo wa Mungu nikafanikiwa kujifungua salama, nawashukuru pia hospitali ya muhimbili kwa jitihada walizofanya kufanikisha jambo hilo,”alisema Jonensia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles