24.1 C
Dar es Salaam
Tuesday, October 8, 2024

Contact us: [email protected]

PAC: Trilioni 1.5 hazijaibiwa

mRAMADHAN HASSAN-DODOMA

BAADA ya kelele na mijadala ya muda mrefu kuhusu mahali zilipo Sh trilioni 1.5, Bunge jana limehitimisha rasmi mjadala huo kwa kusema hakuna wizi wa aina yoyote au fedha zilizopotea.

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Naghenjwa Kaboyoka, aliyasema hayo jana bungeni mjini Dodoma wakati akiwasilisha  taarifa ya shughuli za kamati hiyo kwa mwaka 2018.

Kaboyoka alisema kamati ilifanya uchambuzi wa matokeo ya uhakiki wa

tofauti ya Sh trilioni 1.5 kati ya mapato yaliyokusanywa na Serikali ya Sh trilioni 25.3 na fedha zilizotolewa na hazina Sh trilioni 23.7 kama ilivyoripotiwa Juni 20 mwaka 2017 katika sura ya IV ya taarifa ya CAG.

“Uhakiki huu ulipitia upya fedha zilizoidhinishwa na kutolewa katika Mfuko Mkuu kwa mwaka wa fedha 2016/2017 na 2017/2018.

Aidha, alisema uhakiki huu ulifanyika ili kuthibitisha endapo fedha zilizotolewa kutoka mfuko mkuu zilitoka kwa kuzingatia Katiba na Sheria ya Fedha ya mwaka 2004.

Mwenyekiti huyo alisema uhakiki huo umethibitisha kutokuwepo wa taarifa tofauti ya Sh trilioni 1.5 kati ya makusanyo na mapato ya Serikali katika Mfuko Mkuu kwa mwaka wa fedha 2016/2017.

“Kwa kuwa CAG amekamilisha uhakiki wa mfuko mkuu wa Serikali kwa

mwaka wa fedha unaoishia Juni 2017 na kutoa taarifa yake kwa Bunge,” alisema.

Kaboyoka alisema ili kutekeleza jukumu la uchambuzi wa taarifa hiyo kwa ufanisi, Januari 24, 2019, Kamati ilifanya mahojiano ya kina na CAG ili kupata ufafanuzi wa kina wa taarifa ya uhakiki.

“Aidha, Januari 25, 2019, Kamati ilifanya mahojiano na Katibu

Mkuu, Wizara ya Fedha na Mipango, maofisa kutoka wizara hiyo, Mamlaka

ya Mapato Tanzania (TRA) na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ili kupata ufafanuzi na maelezo ya ziada kwa hoja zilizokuwa zimejitokeza katika

taarifa ya uhakiki.

MATOKEO

Kaboyoka alisema katika uchunguzi sababu ya tofauti ya Sh trilioni 1.5 inayotokana na makusanyo la Sh trilioni 25.3 na fedha zilizotolewa na

Hazina kiasi cha Sh trilioni 23.8 kama ilivyoripotiwa na CAG katika

ripoti ya Hesabu za Serikali Kuu iliyoishia Juni 30 mwaka 2017, CAG alifanya uwianisho kamili wa tofauti za takwimu hizo mbili.

“Uongozi wa Hazina uliwasilisha kwa CAG marekebisho ya takwimu za

hesabu ambazo baada ya ukokotozi na usuluhishi wa taarifa za hesabu za

mapato na matumizi ya Serikali suala la tofauti ya Sh trilioni 1.5

kati ya makusanyo na matumizi ya Serikali halikuwepo kwenye Mfuko Mkuu wa Hazina ya Serikali.

Alisema suala la fedha za ziada zilizotolewa zaidi ya makusanyo, zaidi ya Sh bilioni 290.13, ambapo maelezo ya hazina yalitofautiana

kuwa fedha hizo za ziada zilikuwa ni fedha zilizotumwa moja kwa moja

kwenye miradi.

Aidha, Hazina walifafanua kuwa utolewaji huo wa fedha zaidi ya mapato

ni kwa mujibu wa kifungu cha 34 cha Sheria ya Benki Kuu ya mwaka 2006

kinachoruhusu benki hiyo kupitia Serikali wigo wa kutumia fedha zaidi ya mapato yaliyopatikana.

Alisema kwa mwaka 2016/2017, wigo ulikuwa umetolewa na Benki Kuu ulikuwa Sh bilioni 1.706.46, hivyo utolewaji huo wa fedha za ziada ulikuwa ndani ya wigo wa kisheria.

Aidha, Kaboyoka, alisema uchambuzi wa kamati umebaini kuwa mkanganyiko wa awali uliokuwa umejitokeza ulitokana na kutofanyika marekebisho kwa wakati ya taarifa zinazohusiana na Mfuko Mkuu ambazo ni muhimu katika kusuluhisha hesabu.

“Mathalani uhakiki ulibaini kuwa baadhi ya taarifa muhimu hazikuwa

zimeunganishwa wakati wa kutoa salio la Mfuko Mkuu hivyo kuleta

utofauti wa takwimu.

“Pia usuluhisi wa hesabu ulichelewa kufanyika katika masuala kama

kutothibitisha kwa kiasi cha fedha kilichopo benki, mapato ya fedha

yaliyokusanywa mwaka wa fedha 2016/2017 ambayo yalihamishiwa baada ya Julai 2017.

“Kuchelewa kurekebisha na kuhamisha hawala za Serikali

zilizoiva na kutofautiana katika taarifa zilizomo katika taarifa ya

utekelezaji wa bajeti ya robo ya mwisho iliyotumika kuanza ripoti ya ukaguzi wa mwaka ya CAG na rasimu ya mwisho ya ripoti ya utekelezaji wa bajeti.

“Katika kuhitimisha suala la tofauti ya Sh trilioni 1.5 kati ya mapato ya Serikali na makusanyo kwa mwaka wa fedha 2016/2017, naomba kuweka kumbukumbu sahihi katika Bunge lako  tukufu kuwa tofauti hiyo haikuwepo baada ya marekebisho ya hesabu kufanyika,” alisema.

USHAURI

Kaboyoka alisema ili kuimarisha usimamizi, udhibiti usahihi wa

kumbukumbu na uendeshaji wa mfuko huo, menejimenti imetakiwa kuboresha mfumo wa utunzaji kumbukumbu kwa nyaraka za mfuko kuhifadhiwa katika namna itakayorahisisha rejea.

Pia Wizara ya Fedha na Mipango itoe taarifa za fedha za mfuko mkuundani ya mwaka husika bila kuchelewa na CAG apate fursa ya kutoa maoni

“Hazina ianze kuandaa taarifa ya kila fedha ya mwezi na kuipeleka kwa

CAG ikionesha kwa kina fedha iliyopokelewa na kuhamishwa kutoka mfuko mkuu kuanzia siku ya kwanza ya mwaka wa fedha hadi siku ya mwisho ya

mwezi.

Pia wizara ya fedha na mipango ihakikishe inagawa fedha katika kifungu

kwa kulingana na Sheria ya Bajeti ya mwaka 2015 na ugawaji huo

ujumuishe taarifa ya mgawani wa vifungu kila mwaka.

Aidha, ofisi ya Taifa ya Ukaguzi na Hazina waendelee kushirikiana kwa karibu katika kusimamia uendeshaji wa mfuko mkuu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles