31 C
Dar es Salaam
Tuesday, October 3, 2023

Contact us: [email protected]

P Square wagombana na kaka yao

 P Square wakiwa na Kaka yao Jude Okoye.
P Square wakiwa na Kaka yao Jude Okoye.

LAGOS, NIGERIA

NYOTA wa muziki ambao wanaunda kundi la P Square, Pete na Paul Okoye, wanadaiwa kugombana na kaka yao, Jude Okoye ambaye alikuwa ni mtayarishaji wa kazi zao akiwa kama prodyuza.

Inadaiwa kwamba ndugu hao wamekuwa hawana maelewano kwa muda sasa, hivyo P Square wameamua kuacha kufanya kazi na kaka yao na sasa wanafanya wenyewe.

Kupitia akaunti ya Instagram ya Pete, alidai kwamba wawili hao wamechoka kugombana na kaka yao kila siku tangu Machi mwaka huu, hivyo ni bora wafanye kazi wenyewe.

“Tumekuwa na mgogoro kwa kipindi kirefu na kaka yetu na kuwafanya mashabiki wetu wawe na wakati mgumu, hivyo tumeona bora tufanye maamuzi magumu kwa ajili ya kuweka sawa muziki wetu, tunajua tutakuwa tumewakosea baadhi ya watu ila imebidi tufanye hivyo tunaamini hatuwezi kufanya kazi pamoja kwa kipindi kirefu,” aliandika Peter Okoye.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles