25.6 C
Dar es Salaam
Sunday, January 5, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

P. Diddy hana mpango wa kuoa

P.Dippy-wallpapersBADI MCHOMOLO NA MTANDAO
MSANII tajiri nchini Marekani, Sean John ‘P. Diddy’, amesema hana mpango wa kuoa kwa sasa ingawa anaishi na Cassie kwa miaka nane hadi sasa katika uhusiano wao wa kimapenzi.
Msanii huyo ana watoto watano wakiwemo wawili wa mpenzi wake, Cassie.
Kiongozi huyo wa kundi la Bad Boy mwenye umri wa miaka 45, amesema wanachama wa kundi hilo hawakatazwi kuishi bila ya kuoa.
“Sijui kama nitakuja kuoa, huo ni utaratibu wa maisha yangu nadhani mtu unatakiwa kuwa tayari kwa kuwa moyo utapenda kufanya hivyo. Sitaki kuutesa moyo wa mtu, kila mtu anatakiwa kuwa huru na ndio maana naona bora niishi kama Kurt Russell.”
Russell ni mwigizaji maarufu nchini Marekani ambaye aliishi na mpenzi wake Goldie Hawn kwa miaka 32 bila ya kuoana. Hivyo ndivyo anavyotaka P.Diddy ambaye amefafanua zaidi kwamba akitaka kuoa ataoa kwa mkataba ukiisha wanaachana ama wanaendelea kulingana na makubaliano yao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles