P.Diddy abadilisha jina tena

0
817

LOS ANGELES, MAREKANI

RAPA Sean Combs maarufu kwa jina la P.Diddy, ametangaza kubadilisha jina lake la kati ‘John’ na kuitwa Love au Brother Love kutokana na kubadilisha mfumo wa maisha yake.

Jina lake kamili ni Sean John Combs, lakini ameamua kulitoa John na kuliweka Love, akidai kwa sasa hayupo tayari kutumia majina aliyokuwa anayatumia kama vile P.Diddy, Puffy, Diddy na Puff Daddy.

“Nimeamua kubadilisha jina langu kwa mara nyingine, hii ni kwa sababu maisha yangu kwa ujumla yamebadilika, hivyo kuanzia sasa nitakuwa naitika kwa jina la Love au Kaka Love, ila majina mengine hapana,” alisema msanii huyo.

Hii sio mara ya kwanza kwa msanii huyo kufanya hivyo, Novemba 2017 staa huyo wa muziki wa hip hop alitangaza kubadilisha jina na kuitwa Brother Love, akidai kuwa anapenda sana.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here