26.5 C
Dar es Salaam
Tuesday, January 18, 2022

OZIL: SIJALI WANAONIBAGUA ARSENAL

LONDON, ENGLAND


KIUNGO mshambuliaji wa klabu ya Arsenal, Mesut Ozil, ameweka wazi kuwa hana wasiwasi na maneno ya kibaguzi kutoka kwa mashabiki wa timu hiyo.

Nyota huyo amekuwa akishambuliwa na mashabiki wa timu hiyo kutokana na kugoma kuongeza mkataba mpya, huku mkataba wake wa sasa ukitarajiwa kumalizika 2018, hivyo wanaamini kuwa ataondoka mara baada ya kumalizika kwa msimu huu.

“Bado nina mkataba na klabu ya Arsenal hadi pale 2018, hivyo kwa sasa siwezi kusema kama nataka kuondoka, lakini kila kitu kitakuwa wazi baada ya kumalizika kwa mkataba wangu, bado najitoa kwa ajili ya timu yangu.

“Soka sijaanza leo, hivyo nimekuwa nikikutana na changamoto mbalimbali na sishangai kuona baadhi ya mashabiki wa Arsenal wakionesha ubaguzi, hiyo ni karibu kila sehemu na kila klabu lazima utakutana na watu ambao wanakuwa tofauti na wewe, ninachokiangalia kwa sasa ni jinsi gani nitaisaidia Arsenal katika michezo yake na si kuwafikiria wanaonizungumzia,” alisema Ozil.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
174,926FollowersFollow
531,000SubscribersSubscribe

Latest Articles