23 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

OSHA yafanya maboresho sheria utoaji tozo

Mwandishi wetu-Dar es salaam

KATIKA kutekeleza dira ya maendeleo ya mwaka 2025 ambayo ni kujenga uchumi wa viwanda, Wakala wa Usalama wa Afya Mahali pa Kazi (OSHA),  imeyataja maeneo saba ambayo imeyafanyia maboresho katika utoaji wa huduma zake.

Akitaja maeneo hayo, Kaimu Mtendaji Mkuu OSHA, Hadija Mwenda alisema wamefanya maboresho ya sheria kuhusiana na tozo na ada.

“Tayari tumeziondoa tozo za ada ya usajili wa eneo la kazi ambayo ilikuwa ikitozwa kati ya Sh 50,000 mpaka 1,800,000, ada ya fomu ya usajili sehemu za kazi iliyokuwa ikitozwa Sh 50,000, ada ya leseni  na tozo za ushauri wa kitaalamu,” alisema.

Hadija alitaja eneo jingine  lililofanyiwa maboresho kuwa ni  uondoaji wa urasimu wa utoaji huduma, ambapo OSHA imepunguza muda wa  kupata cheti cha usajili kutoka siku 14 hadi moja.

Pia kupunguza muda wa kushughulikia leseni ya afya mahala pa kazi kutoka siku 28 hadi tatu.

“Eneo la tatu usimikaji wa mifumo ya Teknolojia ya Habari na  Mawasiliano (Tehama) ambapo kupitia mfumo huu usajili wa  maeneo mahala pa kazi utafanyika kwa njia ya kieletroniki, hivyo kuongeza huduma na kupunguza mlolongo wa kupata cheti,” alisema.

Alisema sehemu ya nne ambayo OSHA imefanyia maboresho ni kuongeza uwajibikaji ambapo sasa imeanzisha dawati la kushughulika na malalamiko ya wadau pamoja na kuwepo kwa utaratibu wa wakaguzi wake kufanya ukaguzi kwa timu badala ya mkaguzi mmoja mmoja.

“Eneo la tano ni kuweka utaratibu wa ukaguzi kupitia makao makuu ya taasisi ambapo OSHA imeendelea kuwahamasisha wafanyabiashara na kampuni za uwekezaji zenye ofisi na matawi mengi katika mikoa mbalimbali nchini ili  kuratibu shughuli za ukaguzi, mafunzo na upimaji afya kupitia ofisi ya makao makuu,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles