30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 23, 2024

Contact us: [email protected]

OPERESHENI TOKOMEZA BANGI YAFYEKA HEKARI 31

Colorado and Washington approve marijuana legalization

Na ELIYA MBONEA -ARUSHA

JESHI la Polisi mkoani Arusha kwa kushirikiana na vyombo vingine vya usalama, wamekamata gunia 58 za dawa za kulevya aina ya bangi, kilogramu 210 za mbegu na kuharibu hekari 31 za zao hilo wilayani Arumeru mkoani hapa.

Operesheni hiyo iliyofanyika Januari 10 na 12, mwaka huu ilihusisha vijiji viwili vya Kisimiri Juu na Engaloami -Mwandeti yakiwa ni baadhi ya maeneo maarufu yenye mashamba ya kilimo cha bangi wilayani hapo.

Akizungumzia operesheni hiyo jana mjini hapa, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo, alisema  wataendelea na zoezi hilo linalolenga kuharibu dawa hizo za kulevya kabla hazijaingizwa sokoni.

“Operesheni ya juzi katika Kijiji cha Kisimiri Juu, tulikamata gunia 31, mbegu kilogramu 210 na kuharibu hekari 19 za zao la bangi iliyolimwa. Katika Kijiji cha Engalaomi tulichoma moto gunia 17 na kufyeka hekari 12 za zao hilo,” alisema Kamanda Mkumbo.

Kutokana na kuendelea kushamiri kwa kilimo hicho hasa wilayani Arumeru, Kamanda Mkumbo alisema ili kukomesha vitendo hivyo jeshi hilo litaanza kuwakamata viongozi wa maeneo hayo kwa kushindwa kusimamia.

“Hawa viongozi wa chini wanajua kinachoendelea katika maeneo yao. Lakini wameshindwa kusimamia wajibu wao, sasa tutaanza kuwakamata kwa kushindwa kutekeleza wajibu wao katika maeneo ya kazi,” alisema Kamanda Mkumbo.

Pamoja na kufanyika operesheni hiyo iliyohusisha zaidi ya askari 40 wenye silaha za moto wanaowasili katika vijiji hivyo mapema alfajiri, bado baadhi ya wananchi hupata taarifa za ujio huo na huyakimbia makazi yao huku wakiwaacha wagonjwa na watoto.

Tayari Mkuu wa Kitengo cha Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini,  Kamishna Msaidizi Mwandamizi, Mihayo Msikela, aliitaja baadhi ya mikoa inayoongoza kwa kilimo cha bangi nchini kuwa ni Arusha,  Mara, Morogoro, Iringa na Tanga.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles