28.6 C
Dar es Salaam
Monday, December 9, 2024

Contact us: [email protected]

Operesheni sangara yamkera Dk. Bashiru

NA FLORENCE SANAWA- MTWARA


KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Bashiru Ally, amekerwa na tabia ya baadhi ya wasimamizi wa operesheni sangara inayoendeshwa Kanda ya Ziwa kutotumia mwanya wa usimamizi wa sheria badala yake kunyanyasa wananchi.

Kauli hiyo aliitoa jana mkoani Mtwara wakati akizungumza na wananchi ambapo alisema kuna wasimamizi wahuni.

Alisema maofisa hao wamekuwa wakiwatesa na kuwabughudhi wananchi wakati wanajitafutia riziki bila kuzingatia sheria kwa misingi ya haki.

Dk. Bashiru alisema Waziri wa Uvuvi, Luhaga Mpina, anapaswa kuangalia jambo hilo ili watumishi hao wasimamie sheria kwa misingi ya haki.

“Unajua nasema hivyo, wasimamizi wote wa sheria watambue kuwa nchi inasimamiwa kwa misingi, kwa mujibu wa sheria na usimamizi wa sheria bila kuvunja misingi ya utu,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles