25 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

OPERESHENI MKAA KUTIKISA WIKI IJAYO

Na ASHA BANI


WAKALA wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) itaanza operesheni ya kuimarisha utekelezaji wa sheria za usafirishaji wa mazao ya misitu hususan mkaa wiki ijayo, kwa lengo la kuwahimiza wananchi wafuate kanuni na sheria hizo.

Mkurugenzi wa Mipango na Matumizi endelevu ya misitu na nyuki nchini, Mohamed Kilongo, alisema ataongoza timu ya pamoja ya maofisa wa polisi, Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra) na TFS, kutekeleza operesheni hiyo endelevu kwenye mikoa yote ya Tanzania Bara kuanzia Aprili 10, mwaka huu.

Alisema lengo ni kuhakikisha ufuataji wa mwongozo wa uvunaji endelevu wa mazao ya misitu, sheria za misitu, sheria ya usalama barabarani na kanuni ya utoaji wa leseni za usafirishaji. 

Aliongeza kuwa wamefanya kampeni ya kutoa elimu kwa zaidi ya wiki tatu kuhusu usafirishaji wa mazao ya misitu hususan mkaa, baada ya kubaini kuwa ndicho kichocheo kikubwa cha uharibifu wa mazingira kutokana na kuvunwa kinyume na taratibu kusafirishwa kwa kutumia pikipiki na baiskeli, jambo ambalo ni kinyume na sheria.

Kilongo alisema kulingana na sheria za nchi zilizopo, pikipiki haziruhusiwi kusafirisha mazao ya misitu hususan mkaa, usafirishaji wa mazao ya misitu kwa baiskeli na pikipiki kwani vinakiuka sheria.

Alisema mwongozo wa uvunaji endelevu wa mazao ya misitu wa mwaka 2015, unaeleza kuwa vyombo vya usafiri vinavyoruhusiwa kusafirisha mazao ya misitu ni vile vyenye magurudumu manne.

 Aidha, Sumatra chini ya Kanuni ya Transport Licensing (Motor cycle and Tricycles) ya mwaka 2010, inatambua pikipiki kama chombo cha kusafirisha abiria na si vinginevyo. Huku, Sheria ya Usalama Barabarani sura ya 168 iliyorejewa mwaka 2002, inatambua pikipiki na baiskeli kama vyombo vya usafiri kwa ajili ya abiria na si kubeba mizigo.

Aliongeza kuwa kwa tathmini ambayo wamefanya, pikipiki na baiskeli zinachangia uvunaji haramu na usafirishaji wa haraka wa mazao ya misitu hususan mkaa na inakadiriwa kuwa pikipiki 20 zikisafirisha mkaa ni sawa na lori moja la tani 7 lililojaa mkaa.

“Njia hii ya usafiri inahatarisha maisha ya watumiaji wengine wa barabara na wale waoaoendesha vyombo hivyo.. njia hii ya usafiri inachangia ukwepaji wa makusanyo ya maduhuli ya Serikali.

“Sasa kwenye kampeni ambayo tumeifanya ya kuelimisha wanaosafirisha mkaa kwa pikipiki na baiskeli kwa muda wa zaidi ya wiki tatu, ilikuwa ni kuwaelimisha wananchi sheria zinasemaje ambazo zinatuongoza katika maisha ya kila siku sasa kinachofuata ni sheria kutekelezwa,” alisema Kilongo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles