33.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Ongezeko uuzaji dawa nguvu za kiume unachangia udhalilishaji

KHAMIS SHARIF-ZANZIBAR

IMEELEZWA kuwapo matangazo ya uuzwaji wa dawa za kuongeza nguvu za kiume kiholelo, ni moja  ya sababu zinazochangia kuongezeka vitendo vya udhalilishaji kijinsia dhidi ya wanawake na watoto.

Kauli hiyo, ilitolewa wakati wa tamko la pamoja kwa taasisi  mbalimbali ambazo ni wadau wa kupinga udhalilishaji katika maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia nchini, Kikwajuni mjini Unguja jana

Akiwasilisha tamko hilo kwa waandishi wa habari, Jamila Mahmoud Juma   kutoka Chama cha Wanasheria Wanawake Zanzibar (ZAFELA), alisema kumekua na idadi kubwa ya matangazo katika vyombo vya habari kutangaza matumizi ya dawa kuongeza nguvu za kiume kiholela, huku ikibainika watumiaji si waathirika wa matatizo hayo.

Alisema  wakati mwingine nguvu hizo husababisha kutumika kinyume na sheria na taratibu, hali ambayo husabaisha udhalilishaji unaoshuhudiwa siku hadi siku.

‘’Kuna juisi za tende siku hizi zinatangazwa, viagra, kahawa maarufu kama ‘alkasusi’ inayosemekana inachochea nguvu za kiume, jamii haijiulizi nguvu hizo zikiongezeka zinatumika wapi, kwa binaadam au wanyama? Tunaziomba mammlaka zifanye uchunguzi wa matumizi ya dawa hizi,’’alisema.

Pia aligusia kuibuka wahadhiri wa dini wanaotoa maneno ya kashfa na yasiofaa kimaadili, bila ya kuangalia nani na nani atakayesikia ujumbe huo.

Alisema wengine wanafundisha namna ya kuaminiana kimapenzi na mke na kutoa mada za namna ya mwanamke pekee anavyopaswa kumshughulikia mume.

Washiriki wa mkutano huo, walisema ‘’kuna sheikh mmoja anasema hadharani, eti anapenda mwanamke mwenye umbile fulani, sasa wanaomsikiliza wafanye nini,’’ alisema.

Alisema ni uwazi usiopingika,hivi sasa kada ya dini imevamiwa na kunatolewa mihadhara ambayo ina mkashifu mwanamke pasipo kuangaliwa kwa namna gani wanaiathiri jamii.

‘

Mchangiaji  Malik Shahraan kutoka Zanzibar Cable TV  alisema Serikali na wadau wengine wa kupinga vitendo hivyo wanapaswa kuwa makini pamoja na kuwachukulia hatua stahiki wote watakaohusika.

Tamko hilo, limetolewa na taasisi kama Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA) Zanzibar, Chama cha Wanasheria Wanawake Zanzibar (ZAFELA), Jumuiya ya Wanawake wenye ulemavu Zanzibar na ZAFAKH  ambazo kwa pamoja zinalengo la kupambana na vitendo vya udhalilishaji.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles