27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, February 8, 2023

Contact us: [email protected]

Omog: Ushindi changamoto kwetu

joseph-omog1Na THERESIA GASPER-DAR ES SALAAM

KOCHA Mkuu timu ya Simba,  Mcameroon Joseph Omog, amesema ushindi wa bao 2-1 walioupata katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Ruvu Shooting, umewapa changamoto ya kuendelea kujiandaa zaidi ili kufanya vizuri na si kubweteka.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Omog alisema watapambana kuhakikisha wanapata ushindi katika mechi inayofuata Jumapili dhidi ya Mtibwa Sugar.

“Tunashukuru tumepata pointi tatu muhimu  kwenye mchezo huo, sasa hivi wachezaji wote wanaendelea na mazoezi kwa ajili ya kujiwinda na mchezo wetu unaotukabili mbele yetu dhidi ya Mtibwa Sugar,” alisema.

Kocha huyo raia wa Cameroon, alisema mchezo ujao anaweza kumtumia mchezaji wake, Janavier Bukungu, baada ya kukamilisha hati yake ya uhamisho wa kimataifa ‘ITC’ na kuongezea nguvu kwenye kikosi hicho.

“Bukungu anakuja kuongeza nguvu, natumai tayari ameshaona moto uliokuwepo hivyo atakuja akiwa na nia ya kufanya vizuri na kusaidia timu,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,871FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles