30.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Omog kurudisha hadhi Simba hivi

Joseph Omog
Joseph Omog

NA WINFRIDA NGONYANI, DAR ES SALAAM

KATIKA kile kinachodaiwa kutaka kuisuka upya timu ya Simba, kocha mkuu wa timu hiyo Mcameroon, Joseph Omog, ametaja mambo saba atakayoyazingatia kurudisha timu hiyo katika hadhi yake, MTANZANIA limegundua.

Simba imejichimbia mkoani Morogoro ilikoweka kambi ya kujiandaa na michuano ya Ligi Kuu Tanzania Bara msimu ujao, inayotarajia kuanza mapema Agosti mwaka huu, ikiwa chini ya Omog akisaidiwa na Mganda, Jackson Mayanja.

Omog ambaye ameingia mkataba wa miaka miwili kukinoa kikosi cha Msimbazi, aliwahi pia kuipa ubingwa Azam FC kwa mara ya kwanza katika msimu wa mwaka 2013/14, hivyo ameonekana wazi kuwa na uchu wa kutaka kuudhihirishia umma na wadau wa soka kwa ujumla kuwa yeye ni bora.

Miongoni mwa mambo ambayo Omog amepanga kuyafanya katika kambi ya timu hiyo huko mkoani Morogoro, ni pamoja na  kuhakikisha anakinoa vema kikosi cha timu hiyo ambacho bado kinaendelea kuleta wachezaji kadhaa ili kukiongezea nguvu.

Omog pia amepanga kukiandaa kikosi chake kucheza kitimu, kwa kuhakikisha kuwa wachezaji wanakuwa na ushirikiano wa kutosha ikiwa ni pamoja na kuwa na juhudi binafsi hasa wanapokuwa uwanjani.

Mkakati wake mwingine ni pamoja na kuwaangalia kwa umakini wa hali ya juu, wachezaji anaoletewa na kuwapima kwa kuangalia wachezaji wenye tija na si bora mchezaji jambo alilodai kuwa kwa namna moja ama nyingine litaleta ustawi katika kikosi chake.

Mcameroon huyu pia amepanga kuhakikisha kuwa anakisoma kikosi cha Simba kwa kuangalia na kujifunza makosa ya nyuma ambayo Simba imekuwa ikiyafanya na kuujua vema mtandao wa uongozi wa klabu hiyo ili aweze kupendekeza nini cha kufanya.

Kocha Omog analenga kuifanya Simba kuwa timu ya ushindani, akimaanisha kuifanya kuwa bora zaidi hadi kufikia hatua ya kuogopwa na timu nyingine na iweze pia kujiandaa kucheza michezo kimataifa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles