24.1 C
Dar es Salaam
Sunday, September 8, 2024

Contact us: [email protected]

Ommy Dimpoz amgusa Foby

NA GLORY MLAY

MSANII wa Bongo Fleva, Frank Fedrick maarufu kwa jina la Foby, amedai Ommy Dimpoz ni msanii mwenye mpangilio sahihi wa maneno katika tungo zake.

Foby alisema wapo wasanii wengi ambao wanafanya vizuri hasa kwa kuburudisha, lakini ni wachache ambao wanaweza kupangilia maneno.

“Ommy Dimpoz ni msanii mwenye uelewa mkubwa wa kuandika wimbo anajua mpangilio wa maneno yake kwenye wimbo, wengi wanajua kuandika nyimbo kwa ajili ya kufurahisha mashabiki lakini mpangilio wao ni mbovu.

“Natamani kufanya kazi na msanii huyo hasa kumuandikia wimbo kwa kuwa najua anathamini mchango wa mwenzake, kwa kufanya hivyo ninaamini atanitaja kuwa nimemuandikia, lakini wengine hawawezi kukutaja kwa kuwa hawathamini mchango wako,” alisema Foby.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles