26.9 C
Dar es Salaam
Monday, December 9, 2024

Contact us: [email protected]

Omari K afichua sababu ya kumshirikisha Khadija Kopa

Na Mwandishi Wetu

Siku chache baada ya kuachia wimbo unaoitwa Nanaa, msanii nyota kutoka Kentucky nchini Marekani, Omari K, ameweka wazi siri iliyofanya amshirikishe Malkia wa Mipasho nchini, Khadija Kopa.

Akizungumza na MtanzaniaDigital, Omari K ambaye ana asili ya Kenya amesema mama yake mzazi alikuwa shabiki mkubwa wa Khadija Kopa ndio maana akamshirikisha Malkia huyo wa Taarabu na anawashukuru mashabiki wameupokea vizuri wimbo huo kwenye mitandao mbalimbali.

“Wakati nakua nakumbuka mama yangu aliwakuwa anapenda sana kusikiliza Taraabu na alikuwa anasikiliza nyimbo za Khadija Kopa ndio maana niliamua kumshirikisha kwenye Nanaa.

“Wimbo huu umefanyika Marekani na Tanzania, video imetengenezwa na kampuni mbili za Kwetu Studio ya Tanzania na H Mullah ya Marekani, hivyo naomba sapoti zaidi kwa mashabiki zangu na wa Khadija Kopa ili muziki wangu uzidi kukua,” amesema Omari K.

Akuzungumzia chanzo cha yeye kuingia kwenye muziki, Omari K amesema kuwa wasanii wa Tanzania, Khery Sameer Rajab, maarufu Mr Blue, Diamond Platnumz na Alikiba ndio walimshawishi kuingia kwenye sanaa hiyo kutokana na ukubwa wa kazi zao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles