24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Ole Nasha: Serikali imeimarisha usimamizi matumizi salama ya nyuklia nchini

Mwandishi Wetu, Arusha

Serikali imesema imefanikiwa kuimarisha usimamizi na udhibiti wa matumizi ya Teknolojia ya Nyuklia nchini sanjari na kufadhili miradi mbalimbali katika sekta ya afya.

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Tekenolojia, William Ole Nasha amesema hayo leo Jumatatu Machi 11, wakati wa mkutano wa kimataifa wa waratibu wa miradi ya Sayansi na Teknolojia ya Nyuklia kutoka nchi 49 wanachama wa Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomiki (IAEA) ambapo Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC) ndiyo mwenyeji wa mkutano huo.

Ole Nasha amesema shirika hilo licha ya kufadhili miradi mingi katika sekta mbalimbali hapa nchini ikiwamo sekta ya afya pia imewezesha kupatikana kwa vifaa mbalimbali vya uchunguzi wa tiba na maradhi ya saratani ambavyo vimefungwa katika hospitali ya Rufaa Bugando jijini Mwanza na Hospitali ya Ocean Road jijini Dar es salaam.

“Tunaipongeza TAEC kwa kuendelea kuimarisha ushirikiano baina ya mataifa wanachama hususan kwa utaratibu wake wa kuwa na mikutano inayowezesha kubadilishana uzoefu baina ya wanachama.

“Washiriki wa mkutano huu hakikisheni mnafanya majadiliano yenye tija kwa lengo la kusaidia nchi zenu kwenye udhibiti na matumizi salama ya teknolojia ya nyuklia, majadiliano yenu yalenge katika kuhakikisha mionzi na teknolojia ya nyuklia Afrika inatumika vizuri kwa maendeleo,” amesema.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa IAEA, Profesa Shaukat Abdulrazak amesema wataendeela kushirikiana na serikali ya Tanzania katika kuhakikisha matumizi salama ya teknolojia ya nyukilia kwenye sekta mbalimbali ikiwamo sekta ya afya, kilimo, mifugo, maji, viwanda na ujenzi.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania, Profesa Lazaro Busagara amesema taasisi yake imeendelea kudhibiti na kuwachukulia hatua za kuzifungia taasisi zinazokiuka taratibu za matumizi salama ya mionzi na teknolojia ya nyuklia hapa nchini ikiwamo kutokuwa na leseni, kutokuwa na wafanyakazi wenye utaalamu wa matumizi ya mionzi na teknolojia ya nyuklia na mionzi.

Mkutano huo wa siku tano utamalizika Machi 15, mwaka huu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles