25.7 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

OLE NASHA: Ni kosa kusambaza nyaraka za serikali bila idhini kwenye mitandao

Na Asha Bani

Naibu Waziri wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Wiliam Ole Nasha amesema ni kosa kusambaza nyaraka za serikali katika mitandao ya kijamii bila idhini ya Mamlaka husika, hivyo ameagiza kuchukuliwa  hatua za kinidhamu na za kisheria kwa watumishi watakaobainika kusambaza nyaraka hizo . 

Agizo hilo mkoani Morogoro wakati akifunga semina ya mafunzo ya huduma kwa Mteja na Utunzajiwa Kumbukumbu kwa baadhi ya Maafisa wa Wizara hiyo na kusisitiza kuwa  hakuna mtumishi yeyote wa serikali asiyefahamu kuwa kutoa nyaraka za serikali bila idhini ni kosa la jinai.

 “Kumekuwa na usambazaji wa nyaraka za serikali katika mitandao ya kijamii bila idhini na kwa bahati mbaya wakati mwingine unakuta nyaraka imawekwa mhuri wa siri lakini bado unaikuta huko, watumishi wa serikali lazima watambue kuwa kuna utaratibu wa kutoa nyaraka za serikali na kuna sheria ambazo zinawabana wale wote wanaotoa taarifa hizo bila kuidhinishwa”alisema  Ole Nasha.

Ole Nasha amewataka watumishi hao kutambua kuwa hakuna taasisi yeyote inayoweza kufanya kazi bila kuwa na kumbukumbu au nyaraka hivyo amewataka kuhakiksha   utunzaji mzuri na salama wa nyaraka hizo kwani ni nguzo muhimu katika kufanikisha utendaji wa majukumu.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Rasilimali watu  Moshi Kabengwe amesema mafunzo hayo  yametolewa ili kusaidia watumishi kufanya kazi ambazo zitaleta tija kwa jamii inayohudumiwa na na  kuondoa changamoto ambazo zimebainika katika utoaji wa huduma.

Mafunzo hayo yamefanyika kwa siku Tano na yameshirikisha watumishi zaidi ya 50 kutokaWizara ya Elimu, Sayansi ns Teknolojia Makao Makuu, Vyuo vya Ualimu vilivyopo Morogoro na baadhi ya watumishi kutokaChuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (SUA)

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles