25 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

OJADACT watoa mafunzo ya Sensa kwa Waandishi wa Habari Kanda ya Ziwa

Na Clara Matimo, Mwanza

Chama cha Waandishi wa Habari wa Kupiga Vita Matumizi ya Dawa za Kulevya na Uhalifu Tanzania(OJADACT) kimetoa mafunzo  ya siku moja kwa waandishi wa habari 25 kutoka Mikoa ya Kanda ya Ziwa jinsi ya kuandika habari mwendelezo za sensa.

Akizungumza wakati wa mafunzo hayo yaliyofanyika Agosti 20, 2022 katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza, Mwenyekiti wa OJADACT, Edwin Soko amesema mafunzo hayo ni matokeo ya utafiti walioufanya Julai na Agosti, 2021 kuhusu habari za mwendelezo wa sensa zinazoandikwa na waandishi baada ya zoezi la sensa kupita.

Baadhi ya waandishi wa habari waliuoshiriki mafunzo ya jinsi ya kuandika habari mwendelezo za sensa jijini Mwanza Agosti 20,2022 mafunzo hayo ya siku moja  yaliandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari wa Kupiga Vita Matumizi ya Dawa za Kulevya na Uhalifu Tanzania(OJADACT).

“Katika utafiti huo tuligundua kuna ombwe kwamba waandishi wa habari inapokuja sensa ndiyo wanashirikishwa na wanashiriki kikamilifu lakini likipita zoezi la sensa na waandishi wanakwenda likizo wanakuja tena kuanza kuandika habari za sensa baada ya miaka 10 hali hiyo imekuwa haina tija kwenye tasnia ya habari.

“Baada ya kubaini changamoto hiyo tukaona tuandae mafunzo haya mkoani Mwanza ingawa siku zimebaki chache kufikia siku ya sensa, lakini tunaamini waandishi hawa tutakaowafundisha leo watakuwa na uwezo wa kuandika habari za mwendelezo kuhusu zoezi hilo hasa kwa kuzingatia umuhimu wa sensa ndani ya taifa letu,” amesema Soko na kuongeza:

“Tunatarajia waandike nini maana ya tija ya sensa, mwitikio wa wananchi ulikuwaje, kasoro zilizojitokeza  ili serikali ijiandae kuboresha maeneo hayo kwa ajili ya sensa ijayo watakapokuwa wanaandika habari hizo jamii itakuwa inaona umuhimu wa sensa maana inahaki ya kufahamu mbadiliko yaliyopatikana baada ya sensa, nini manufaa ya watu kushiriki zoezi hilo, mwitikio ulikuwaje je huduma za kijamii zimeongezeka kwa kiasi gani huo ni wajibu wetu waandishi wa habari,” amesema Soko.

Mratibu wa OJADACT, Lucyphine Kilanga aamesema lengo la mafunzo hayo ni kuwafundisha waandishi hao namna ya kuendeleza kuandika habari za sensa baada ya zoezi hilo kupita maana kwa kufanya hivyo Serikali itakuwa haitumii nguvu kubwa kuwaelimisha wananchi kama iliyotumia  kwenye sensa ya  mwaka huu 2022 maana kila siku watakuwa wanasoma na kusikiliza mambo mbalimbli ambayo ni matokeo na faida ya sensa. 

Mkuuwa wa Wilaya ya Nyamagana, Amina Makilagi ambaye alikuwa mgeni rasmi katika semina hiyo aliipongeza OJADACT kwa kuandaa mafunzo hayo ambayo yatasaidia kuwajengea uwezo waandishi wa habari ili baada ya sensa waweze kuandika habari mwendelezo wa sensa.

“Kusema ukweli bila kupepesa macho baada ya zoezi la sensa kuisha huwa hakuna habari za sensa zinazoandikwa hata kuhusu mipango endelevu ya maendeleo kutokana na idadi ya sensa kwa hiyo semina hii itasaidia wananchi kutambua umuhimu wa kushiriki kikamilifu katika zoezi la sensa maana kama wananchi wasipotambua umuhimu wa sensa akitokea mpotosha anapata nafasi kuliko sisi watu wengi ambao tunajukumu la kuielimisha jamii kuhusu umuhimu wa sensa.

“Sijafanya utafiti lakini naamini ninyi mnaweza mkawa ndiyo taasisi ya kwanza hapa nchini kuandaa semina kama hii sielewi kwa mikoa mingine lakini kwa Mwanza kwa kweli nawapongeza sana OJADACT  hakika mmeonyesha nyie ni wazalendo maana mnataka ziwepo habari endelevu ili baada ya sensa jamii ijue mafanikio yaliyopatikana kwenye sensa, changamoto zilizojitokeza na faida za sensa,” amesema Makilagi.

Makilagi amesema lengo la sensa ni kuweka mipango endelevu kwa ajili ya taifa hivyo habari endelevu baada ya sensa ni muhimu kwa kuwa jamii itapata elimu kwa ukubwa zaidi ambazo zitakuwa na tija kwa serikali maana waandishi hao watakuwa wanafuaatilia hata miradi ya maendeleo.

Katika semina hiyo waandishi hao walifundishwa mambo mbalimbali yanayohusi mwendelezo wa habari za sensa ikiwemo jinsi ya kuainisha vyanzo vizuri vya  sensa na  jinsi ya kupanua wigo wa habari watakazoziandika.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles