26.9 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

OIL ZA KUPIMA ZAPIGWA MARUFUKU

Na VERONICA ROMWALD– DAR ES SALAAM


KIGWANGALA

SERIKALI imepiga marufuku uuzwaji wa vilainishi (oil) vya magari vya kupima, unaofanyika mtaani na sokoni kwa kuwa vingi vimechakachuliwa.

Imesema vifungashio vya vilainishi hivyo havikidhi ubora, hivyo kuathiri utendaji wa mitambo.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamis Kigwangwala, alisema hayo Dar es Salaam jana alipozungumza na waandishi wa habari.

Alisema Serikali imechukua uamuzi huo kwani imebaini vilainishi vingi havijakidhi viwango vya kitaifa vinavyopendekezwa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS).

“Wizara kupitia Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, inatekeleza jukumu la kusimamia sheria namba tatu ya mwaka 2003 inayohusu usimamizi na udhibiti wa kemikali za viwandani na majumbani.

“Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali ilifanya ufutiliaji wa ubora wa vilainishi vinavyouzwa sokoni na kuvifanyia uchunguzi ili kubaini kama vimekidhi viwango vya ubora,” alisema.

Aliongeza “Vilainishi kadhaa vilivyokamilika (finished Lubricants) vilichukuliwa katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam na kufanyiwa uchunguzi huo ambapo ilibainika asilimia 50 ya vilainishi vya injini ya petroli, asilimia 52.6 ya vilainishi vya injini ya diseli, asilimia 77.7 ya vilainishi vya Automobile Transmission Fluids (ATF) na asilimia 50.6 ya vilainishi vya “Gear oil” ambavyo vilichunguzwa, vilionekana kutokikidhi viwango vya ubora vya vilainishi vya kitaifa,” alisema.

Aidha Dk. Kigwangwala alisema madhara makubwa yanayosababishwa na matumizi ya vilainishi visivyokuwa na ubora ni uharibifu wa mitambo na mashine.

“Lakini pia iwapo vitaenda kuuzwa nje ya nchi na ikagundulika kuwa vimetoka Tanzania, maana yake ni kwamba vinatuharibia sifa ya nchi,” alisema.

Katika hatua hiyo, waziri huyo alimwagiza Mkemia Mkuu wa Serikali, Profesa Samwel Manyele, kuendelea na uchunguzi wa kimaabara kwa vilainishi vilivyopo sokoni, ili kubaini vile halisi na visivyokidhi viwango na ubora.

“Serikali inapiga marufuku uingizaji wa vilainishi vilivyotumika (recycled lubricants) na vilainishi visivyo na ubora nchini, kwani ni kinyume cha matakwa ya sheria,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles