23.3 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

OFISI ZA PSPF TOWERS JIJINI ZAUZWA KWA WALIONAZO

pspf-towers

Na Mwandishi Wetu,

JENGO maridhawa na linaloongoza kwa umaridadi na uzuri jijini Dar es Salaam, sehemu kuu ya biashara (CBD) ambayo ni ya PPF Towers linauzwa kwa walionacho ili kuishi katika jengo la kifahari.

Jengo hili ambalo liliwekwa jiwe la msingi na Rais Mstaafu Jakaya Kikwete  na baadaye lilifunguliwa kwa mbwembwe na Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Demokrasi ya Kongo (DRC) wakati wa ziara yake Tanzania, limeanza kuuzwa na kupangishwa kwa wahitaji.

Jengo hilo linasemekana kuwa ni refu kupita yote Afrika Mashariki, limejengwa kwenye kitovu cha biashara na linatazamana na Bahari ya Hindi kwenye upande wake wa Mashariki linatoa mandhari nzuri ya Jiji la Dar es Salaam na kuliinua hadhi jiji hilo kwa kuwa na jengo lenye hadhi ya kipekee.

Wanunuzi wanakaribishwa wa mataifa yote bila kujali uraia wao ili kuja kupanga au kununua ofisi zake kama zilivyoainishwa kwenye  ramani zake za ujenzi.

Jengo hilo kama linavyoonekana pichani ni la aina yake na mjengo wa kileo wa aina ya ‘slim’ na unapendwa sana katika miji mikuu ya Afrika.

Jengo hilo inauza ofisi zake za kibiashara zenye ukubwa wa mita za mraba 500 hadi 900 kwa kiwango cha bei ya chini kwa kitega uchumi madhubuti  na katika eneo bora kabisa  linalowafaa mabilionea  ambao wanataka  ukimya, amani na utulivu wa mawazo.

Kile kinachouzwa si jengo lote ila kutoka ghorofa ya 22 hadi 31 na kukiwa na mandhari nzuri ya rangi ya bluu ya Bahari ya Hindi.

Jengo hilo limesanifiwa kiustadi ambapo linaruhusu kuwa katika mifumo mbalimbali ya makazi na ofisi kwa matumizi ya kila aina na kadiri mtumiaji anavyotaka.

Vile vile PSPF Towers liko karibu sana na huduma zote muhimu za kibenki, migahawa, maduka makubwa, hoteli  n.k.

Maeneo makuu ya ofisi yako ghorofa ya Mezanine na ghorofa ya chini (GF) ambazo ni bora kwa mabenki na maduka.

Huduma nyingine ambazo ni sehemu ya majengo hayo ni eneo zuri la kuegesha magari, lifti kuelekea kila ghorofa, jenereta ya kusubiria, akiba ya maji ya uhakika, usalama na ulinzi saa 24 na vyote hivyo vinapatikana kwa bei ya dola 2,200 kwa mita ya mraba kwenye eneo la kuanzia mita za mraba 550 hadi  mita za mraba 990.

Jengo lingine la PSPF ni Golden Jubilee Tower la Mtaa wa Ohio jijini Dar es Salaam ambapo zaidi ya wizara tisa zimepanga kwenye jengo hilo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles