30.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Ofisi ya Waziri Mkuu yashiriki Wiki ya Utumishi wa Umma

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Watumishi wa ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu wameaswa kuendelea kufuata maadili ya utumishi Umma kwa kufanya kazi vizuri na kuwa wabunifu katika utendaji wa kazi, ili kuepuka kufanya kazi kwa mazoea.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu, Dk. John Jingu pamoja na Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Dk. Wilson Charles na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu, Kaspar Mmuya wakifutilia kwa umakini semina ya wafanyakazi kwa watumishi wa wizara hiyo iliyofanyika ukumbi wa tume ya Uchaguzi Dodoma.

Hayo yamesemwa leo Juni 22, 2022 na Katibu Mkuu, Dk. John Jingu wakati wa semina kwa wafanyakazi wa Ofisi hiyo yaliyofanyika katika ukumbi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi jijini Dodoma katika kuadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma.

Wiki hiyo imebebwa na kauli mbiu ya: “Nafasi ya Mapinduzi ya nne kwa viwanda katika Masuala mapya yanayojitokeza kuhusu utoaji wa huduma na urejeshwaji wakati na baada ya janga la corona.”

“Serikali kupitia Rais Samia Suluhu Hassani imeshatimiza wajibu wake kwa kuhakikisha maslahi ya wafanyakazi; marupupu, vitendea kazi vinapatikana, jukumu letu ni kuwajibika ipasavyo ili kuhakikisha kwamba wananchi wanafurahia huduma wanayopatiwa na serikali,” amesema Dk. Jingu.  

Alifafanua vikao hivi ni muhimu vinapaswa kufanyika mara kwa mara ili kuweza kujua mipaka ya kiutendaji wa kazi iko wapi. Lazima tufanye kazi kama timu kwa kuzingatia maslahi mapana ya Taifa.

Watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu wa Idara mbalimbali wakifuatilia semina iliyofanyika katika ukumbi wa Tume ya Uchaguzi katika kuadhimisha wiki ya Utumishi wa umma.
Watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu wakisikiliza na kufuatilia kwa umakini, Dk. Revocatus Baltazary  Ofisi ya Mganga Mkuu Jiji la Dodoma (hayupo pichani) katika semina iliyofanyika katika ukumbi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi katika kuadhimisha wiki ya Utumishi wa umma.
- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles