25.2 C
Dar es Salaam
Sunday, August 14, 2022

Ofisi ya Msajili yaanza kuchambua majibu ya ACT

PATRICIA KIMELEMETA – Dar es salaam

OFISI ya Msajili wa Vyama vya Siasa imesema inafanyia kazi barua ya Chama cha ACT-Wazalendo baada ya kutakiwa ijieleze kwanini kisifutwe.

Akizungumza na gazeti hili Dar es Salaam jana, Msajili Msaidizi Sisty Nyahoza, alisema barua hiyo wameipokea wiki iliyopita na tayari imeanza kufanyiwa kazi kwa mujibu wa sheria za vyama vya siasa nchini.

 “Tumepokea barua ya Chama cha ACT-Wazalendo ya kujibu hoja zetu tulizowaandikia kwenye barua yenye kumbukumbu namba HA.322/362/20/98 ya Machi 25, ya kuwataka kujibu hoja mbalimbali ikiwamo ya kutowasilisha hesabu za ukaguzi za 2013/14, hivyo kutokidhi matakwa ya barua ya msajili wa vyama vya siasa, hatua inayokiuka sheria ya vyama vya siasa sura ya 258,” alisema Nyahoza.

Aliongeza kutokana na hali hiyo, barua hiyo itafanyiwa kazi kwa mujibu wa sheria ya vyama vya siasa ili waweze kutoa haki kulingana na matakwa ya kisheria.

Alisema chama hicho kimejibu hoja hizo ndani ya muda uliopangwa wa siku 14 kama walivyoelezwa, hivyo basi wakimaliza kuipitia, watawajibu kwa kufuata taratibu za kisheria.

Awali katika barua ya msajili iliyowasilishwa kwa ACT-Wazalendo wiki mbili, ilieleza kuwa kwanini chama hicho kisifutiwe usajili kutokana na kushindwa kuwasilisha hesabu za ukaguzi za mwaka 2013/14.

Barua hiyo ilieleza kuwa mashabiki wa Maalim Seif ambao wanadai sasa ni wanachama wa ACT-Wazalendo wamefanya vitendo vya uvunjifu wa sheria ikiwamo kuchoma moto bendera za Chama cha Wananchi (CUF) baada ya mahakama kutoa hukumu katika kesi namba 23 ya 2016.

Ilieleza pia kuwa kitendo hicho ni kukiuka kifungu cha 11C cha sheria ya vyama vya siasa.

Tuhuma nyingine ni chama hicho kutumia dini katika siasa zake baada ya mashabiki wake kuonekana katika mitandao wakipandisha bendera ya ACT-Wazalendo kwa kutumia tamko takatifu la dini ya Kiislamu (Takbir), kitendo kinachokiuka kifungu cha 9 (1)(C) cha sheria hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,695FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles