29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Ofisi ya Mkemia Mkuu yatoa tuzo za masomo ya sayansi

Aveline Kitomary

Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, imetoa tuzo Kwa wanafunzi na walimu bora kitaifa waliofanya vizuri sana kwenye somo la Kemia, Fizikia na Baiolojia kidato cha nne na cha sita.

Akizungumza wakati wa kutoa tuzo hizo jijini Dar es Salaam Mkemia Mkuu wa Serikali, Dk. Fidelix Mafumiko, amesema kuwa wametanua wigo katika utoaji tuzo kwa kuongeza somo la Fizikia.

“Tulianza kutoa tuzo kwa wanafunzi waliofanya vizuri kwenye somo la kemia lakini tukaongeza wigo kwa somo la Baiolojia na Fizikia, tuzo za kupongeza walimu na wanafunzi tulizotoa tangu tulipoanza hadi kufikia leo ni Jumla ya wanafunzi 128 na walimu 22.

“Shule zilizofanya vizuri na kuongoza katika masomo hayo ya Kemia, Baiolojia na Fizikia, ni St. Fransinci yenyewe imetoa wanafunzi nane, St. Anne, St Mary’s Ilboru Kilakala, Tabora girls na Fezza boy’s,” amesema Mafuniko.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wazee na watoto, Prof. Mabula Mchembe, amehamasisha wanafunzi kupenda masomo ya sayansi na kuagiza shule kuwa na vifaa vya kufanyia mazoezi.

“Mashuleni kunatakiwa kuwepo na vifaa vyote vya msingi ili kuwasaidia wanafunzi kufanya vizuri na kuwa na uwelewa juu ya kitu wanachofundishwa na sio wanafunzi kujifunza darasani bila vitendo huku mkitegemea wanafunzi kujuwa kwa kusikia wanatakiwa kuona wanachoambia.

“Tumeingia kwenye uchumi wa kati kwa hiyo uahindani ni mkubwa wanafunzi wanatakiwa kusoma kwa bidii, kwa vitendo zaidi nasio bila vitendo. 

“Zawadi zinatolewa ili kusaidia wanafunzi kuwapa motisha katika kusoma kwa bidii pamoja na walimu kuongeza bidii katika ufundishaji hii iongezwe kuwapa wanafunzi wengine waliofanya vizuri kwenye masomo mengine,” amesema Mchembe.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles