23.2 C
Dar es Salaam
Friday, June 9, 2023

Contact us: [email protected]

Ofisi ya Madini Simiyu yaeleza sababu za mgogoro wa wachimbaji Bulumbaka

Na Derick Milton, Simiyu

Ofisi ya Madini mkoa wa Simiyu imesema kuwa mgogoro unaoendelea wa wachimbaji wadogo na kikundi kilichopewa leseni ya kusimamia uchimbaji wa Madini ya dhahabu kwenye mgodi wa Bulumbaka namba mbili katika Wilaya ya Bariadi mkoani humo sababu kubwa ni watu kutokujua Sheria.

Kwa mara ya kwanza ofisi hiyo imezungumzia mgogoro huo ambao umedumu kwa muda mrefu toka mwaka Jana, ambapo Kaimu Ofisa Madini Mkoa, Joseph Kumburu amesema kuwa ofisi yake haina makosa yoyote ambayo iliyafanya kwa kutoa leseni kama watu wanavyosema.

Akiongea na wachimbaji leo katika mgodi huo Kumburu amesema kuwa Ofisi yake ilitekeleza wajibu wake kama ambavyo Sheria inataka, kwa kutoa leseni halali kwa kikundi ambacho kiliomba, lakini suala la wamiliki wa mashamba kukataa kikundi hicho hilo siyo jukumu la ofisi yake.

Amesema kuwa malalamiko yaliyopo na ambayo yanazuia shughuli za uchimbaji kufanyika kwenye eneo lililopewa leseni hiyo, kutoka kwa watu ambao wanajiita wamiliki wa mashamba na hawalushirikishwa kwenye leseni hiyo Jambo ambalo alisema siyo kweli na siyo wamiliki halali wa mashamba hayo.

“Wote wale ambao wanalalamika siyo wamiliki wa mashamba, wamiliki wa mashamba wenyewe tayari wamekubaliana na kikundi ambacho kilipewa leseni, lakini tunashangaa hawa watu na tumegundua wanatumwa kufanya fujo na vurugu na watu wenye maslai yao binafsi,” amesema Kumburu.

Aidha, Ofisa huyo amewaambia Wachimbaji hao kuwa kwa Sasa ofisi yake haijihusishi na mgogoro kwani unashughulikiwa na ofisi ya Mkuu wa pamoja n ofisi ya Mkuu wa mkoa, ambapo aliwataka wachimbaji kuwa na subira wakati viongozi wa mkoa na Wilaya wakiendelea kutafuta suluhisho.

Amesema kuwa kinachofanyika kwasasa ni uhakiki wa wamiliki halali wa mashamba kutoka pande mbili za wachimbaji na kikundi kilichopewa leseni, ambapo baada ya zoezi hilo uhamuzi utatolewa na viongozi ambao wanashughulikia mgogoro huo.

“Sisi kama ofisi ya Madini tulimaliza kazi yetu ya kutoa leseni Kama sheria inavyotaka, hayo mengine ya mgogoro hatuyajui, ofisi ya Mkuu wa mkoa na mkuu wa Wilaya ndiyo wanaendelea kulifanyia kazi, kuna uhakiki unaendelea wa kujua nani mmiliki halali wa mashamba,” amesema Kumburu.

Ofisa Madini huyo ameeleza kuwa kinachosababisha mgogoro huo ni uelewa mdogo wa sheria ya Madini, ambapo aliwataka wachimbaji kusoma vizuri sheria hiyo na kuzifuata ili kutokuzuia shughuli za uchimbaji kufanyika.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,351FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles