27 C
Dar es Salaam
Friday, May 27, 2022

Ofisa waujasusi adai kutishwa na Trump

NEW YORK- MAREKANI

OFISA mmoja wa ujasusi katika Wizara ya Usalama wa Ndani wa Marekani, Brian Murphy, amedai kushinikizwa na shirika la ujasusi la nchi hiyo kuficha tishio la Urusi la kuingilia Uchaguzi Mkuu wa nchi hiyo wa mwaka 2016 ili kumlinda Rais Donald Trump.

Taarifa iliyoripotiwa na vyombo mbalimbali vya habari duniani jana ilieleza kuwa piaMurphy alidai kushushwa cheo kwa kukataa kuzifanyia marekebisho ripoti zinazohusu kashifa hiyo.

Iliongeza kuwa Murphy alikataa kushiriki suala hilo pamoja na mengine kwa sababu maangizo aliyopewa yalikuwa kinyume cha sheria .

Hata hivyo Ikulu ya nchini hiyo (White House) na wizara ya usalama ya ndani imekanusha madai hayo.

Mapema wiki hii Murphy aliituhumu Waziri wa zamani wa wizara ya usalama wa ndani ya Marekani, Kirstjen Nielsen, ambaye kwa sasa ni kaimu waziri wa Chad Wolf na naibu wake, Ken Cuccinelli.

Murphy alisema kati ya Machi 2018 na Agosti 2020, kulikuwa na matukio ya matumizi mabaya ya mamlaka ikiwamo kujaribu kuzuia uchambuzi wa taarifa za kijasusi na utawala usiofaa wa mpango wa ujasusi unaohusiana na juhudi za Urusi za kushawishi na kudhoofisha maslahi ya Marekani.

Taarifa hiyo ilieleza kuwa katikati ya Mei mwaka huu Murphy aliagizwa na Wolf  kuacha kutoa tathmini ya kijasusi juu ya tishio la uingiliaji wa Urusi badala yake aanze kuripoti kuhusu shughuli za uingiliaji wa China na Iran.

Iliongeza kuwa maagizo hayo yalitolewa moja kwa moja kutoka kwa Mshauri wa White House wa Masuala ya Usalama, Robert O’Brien.

Murphy alidai kukata maagizo hayo kwa sababu kufanya hivyo kungeliweka taifa katika hatari kabla ya Julai mwaka huu kuambiwa kuwa ripoti ya ujasusi inapaswakuzuiwa kwa sababu ingemfanya Rais Trump aonekane vibaya.

Murphy alidai kuwa wakati katika kipindi hicho aliondolewa katika mikutano kabla ya Julai kushushwa cheo kutoka kuwa kaimu waziri na Katibu Mkuu wa Wizara hadi Msaidizi wa Naibu Waziri Kitengo cha Utawala nafasi ambayo anataka arejeshewe.

Kwa muda sasa Rais Trump amekuwa akiyapinga madai ya Urusi kuingilia uchaguzi licha ya matokeo ya uchunguzi wa idara ya ujasusi ya nchini hiyo kubaini kuwa Urusi iliingilia, na kuyataja madai hayo kuwa ‘kuwa ni utapeli wenye uchochezi wa kisiasa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
192,454FollowersFollow
541,000SubscribersSubscribe

Latest Articles