23.8 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

OFISA WANYAMAPORI AJERUHI MTU KWA RISASI

Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Rukwa, George Kyando
Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Rukwa, George Kyando

Na WALTER MGULUCHUMA- KATAVI


 

MTU mmoja aliyejulikana kwa jina la Salaganda Kipeta, mkazi wa Tarafa ya Kipeta, Wilaya ya Sumbawanga, Mkoa wa Rukwa, amejeruhiwa vibaya kwa kupigwa risasi mguuni.

Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Rukwa, George Kyando, aliwaambia waandishi wa habari jana kwamba, Kipeta alijeruhiwa na Ofisa Wanyamapori katika Pori la Akiba la Uwanda wa Kipeta, aliyetambuliwa kwa jina la Lemomo Miseyeko.

Alisema kwamba, tukio hilo lilitokea juzi saa saba mchana katika pori hilo la akiba.

“Mwananchi huyo alipigwa risasi baada ya kutuhumiwa kuingia ndani ya msitu wa hifadhi bila kuwa na kibali.

“Katika harakati za kutaka kumkamata, mtuhumiwa alikaidi amri halali iliyomtaka atulie, ndipo ofisa huyo wa wanyamapori alipoamua kumpiga risasi katika mguu wa kushoto na kumjeruhi vibaya.

“Kwa kifupi chanzo cha tukio hilo ni Salaganda kukaidi amri halali ya kumtaka asimame ili akamatwe,” alisema Kamanda Kyando.

“Kwa hiyo yule askari aliyehusika katika tukio hilo, tunamshikilia kwa mahojiano zaidi kwani  alitumia nguvu nyingi zaidi kumdhibiti majeruhi ambaye hakuwa na silaha,” alisema Kamanda Kyando.

Pamoja na hayo, kamanda huyo wa polisi alitoa wito kwa askari wa wanyamapori kuacha  kutumia vibaya mamlaka waliyonayo pindi wanapokuwa wakitaka kuwakamata watuhumiwa.

Pia aliwataka wananchi kuacha tabia ya kuingia  ndani ya hifadhi bila vibali kwa kuwa kufanya hivyo ni kukiuka sheria.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles