20.5 C
Dar es Salaam
Saturday, August 20, 2022

Ofisa wa jeshi Ufaransa atoa ushahidi mpya

KIGALI, RWANDA

OFISA wa zamani katika ngazi ya juu ya Jeshi la Ufaransa, Jenerali Jean Varret, ametoa ushahidi mpya kuhusu msimamo wa Ufaransa wakati wa mauaji ya kimbari dhidi ya Watutsi na Wahutu wenye msimamo wa wastani nchini Rwanda.

Mkuu huyo wa zamani wa ujumbe wa ushirikiano wa kijeshi wa Ufaransa nchini Rwanda, amesema alipinga msaada wa Ufaransa kwa Rais Habyarimana, bila mafanikio.

Kwa mujibu wa ofisa huyo mwenye umri wa miaka 84, mkuu wa polisi ya Rwanda wakati huo, Kanali Pierre-Celestin Rwagafilita, alimwambia mnamo mwaka 1990 kwamba Watutsi walio wachache wanatakiwa “kuangamizwa”. Jenerali Jean Varret, ametoa ushahidi huo kwa wenzetu wa redio France Inter na Mediapart. Ni karibu miaka 25 sasa baada ya mauaji hayo yaliyotokea nchini Rwanda, ambapo Varret anaamua kuvunja ukimya na kusema yaliyotokea huku akieleza jukumu la Ufaransa wakati wa mauaji hayo.

Amerejelea hasa mazungumzo ya ana kwa ana kati yake na ofisa wa polisi wa zamani wa Rwanda, Pierre-Celestin Rwagafilita: “Na hapo, aliniambia: “Tunaongea ana kwa ana, sote hapa ni askari, tunapaswa kuweka mambo yote wazi. Ninakuomba hizo silaha, kwa sababu nitashiriki na jeshi katika operesheni ya kuondoa njiani tatizo hilo.” Niliposhangazwa na kauli hiyo, alisema: “Tatizo hilo ni rahisi sana. Ukweli ni kwamba Watutsi si wengi, tutawaangamiza,” aliniambia wazi.

Kwa upande wa Jenerali Varret, amesema mpango wa mauaji ya kimbari ulikuwepo. Anasema pia kuwa alitoa taarifa hiyo kwa jeshi la Ufaransa, lakini viongozi hawakujibu: “Hakuna. Kwa sababu hawakutaka kuunga mkono mpango huo wa Habyarimana. Kwa bahati mbaya, historia imethibitisha kwamba ilikuwa ni kosa zaidi ya kosa, kwa sababu mauaji ya kimbari yalitokea bila hata hivyo kuzuia kabla hayajatokea wakati taarifa za mpango huo zilikuwepo.

“Mwezi ujao, Rwanda inajiandaa kuadhimisha kumbukumbu ya miaka 25 ya mauaji ya kimbari. Rais wa Ufaransa amealikwa rasmi kwenye sherehe hizo. Elysee mpaka sasa, haijaweka wazi jibu lake. Emmanuel Macron alijibu tu kwamba Ufaransa itawakilishwa.”

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
199,058FollowersFollow
551,000SubscribersSubscribe

Latest Articles