27.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

OFISA UTUMISHI ASIMAMISHWA KWA KUKAIDI KUWARUDISHA WATUMISHI WALIOSIMAMISHWA

Susan Uhinga, Tanga

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Bumbuli, wilayani Lushoto mkoani Tanga, Peter Nyalali, amemsimamisha kazi Kaimu Ofisa Utumishi wa halmasahauri hiyo Protas Dibogo kwa kosa la kukaidi kuwarudisha kazini watendaji wa vijiji 41 licha ya serikali kuagiza warejeshwe.

Nyalali ametoa kauli hiyo wakati wa kikao chake na watumishi wa halmashauri hiyo ambapo pamoja na mambo mengine amesisitiza watendaji hao kwenda kufanya kazi kwa bidii kwenye maeneo yao mara tu watakaporejea kazini.

Hivi karibuni serikali iliagiza kurudishwa kazini kwa watumishi wote walioajiriwa kuanzia Mei Mosi, mwaka 2004, ambapo mara baada ya kauli hiyo Nyalali alimwagiza Dibogo kuwarudisha kazini watendaji hao 41 wa vijiji.

Pamoja na kutolewa agizo hilo Kaimu Ofisa huyo Utumishi anadaiwa kutotekeleza agizo hilo jambo lililomlazimu mkurugenzi kumsimamisha kazi.

Nao baadhi ya watumishi waliokuwa wamesimamishwa kazi kwa miezi minane walitoa shukrani zao kwa serikali na kuahidi kuendelea kuwa wachapakazi.

Mei 2, mwaka 2004 serikali iliwaajiri watumishi waliokuwa wakijitolea katika maeneo mbalimbali nchini na baadaye kutoa kibali cha kuajiri watumishi wapya wenye elimu ya darasa la saba huku ikiwataka kujiendeleza wawapo kazini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles