23.8 C
Dar es Salaam
Friday, September 22, 2023

Contact us: [email protected]

Ofisa Usalama Posta kizimbani

KULWA MZEE-DAR ES SALAAM

JAMHURI imewafikisha mahakamani, Ofisa Usalama wa Shirika la Posta Tanzania, George Mwamgabe (44) na mwenzake, wakikabiliwa na mashtaka mawili ya kusafirisha dawa za kulevya.

Mshtakiwa Mwamgabe na Abrahamani Msimu (54) ambaye ni dereva na mkazi wa Yombo, Dar es Salaam walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jana na kusomewa mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Augustine Mmbando.

Wakili wa Serikali Aldolf Lema, alidai Agosti 25 mwaka jana katika eneo la Posta, Dar es Salaam, washtakiwa hao kwa pamoja walisafirisha dawa za kulevya aina ya bangi gramu 124.55.

Katika shtaka la pili, inadaiwa Agosti 25, 2018 katika eneo la Posta washtakiwa wote kwa pamoja walisafirisha dawa za kulevya aina ya heroin gramu 1.55.

Washtakiwa walikana kutenda makosa hayo, upande wa mashtaka ulidai upelelezi haujakamilika na hakukuwa na pingamizi la dhamana.

Akitoa masharti ya dhamana, aliwataka kila mshtakiwa kuwa na wadhamini wawili, mmoja kutoka ofisi za umma, watakaosaini dhamana ya maandishi ya Sh milioni tano kila mmoja.

Hata hivyo, washtakiwa hao walishindwa kutimiza masharti ya dhamana, hivyo wamerudishwa rumande hadi Oktoba 16 kesi hiyo itakapokuja tena kwa kutajwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,690FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles