23.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Ofisa Mifugo kizimbani kwa tuhuma za kupokea rushwa ya Sh 20,000

Self Takaza, Iringa

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru)  mkoani Singida, imempandisha kizimbani Ofisa Mifugo   wa Halmashauri ya Mkalama kwa kupokea rushwa ya Sh 20,000  ili atoe kibali cha kuuzia nyama.

Mtumishi huyo John Yako (32) ambaye ni Ofisa Mifugo daraja la pili, alipandishwa kizimbani mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Iramba, Sydney Nindi.

Mwanasheria wa Takukuru Mkoani Singida, Mzalendo Widege, akisoma mashitaka alidai Mei 28, 2020 Yako aliomba rushwa ya Sh 20,000  kwa Ramadhani Shumbi kinyume na sheria ya Kuzuia na kupambana na Rushwa kifungu 15(1)na (2)namba 11 ya mwaka 2007.

Widege alidai katika shtaka la pili, mtuhumiwa huyo anadaiwa kuwa Mei 30, 2020 katika Kata ya Ibaga wilayani Mkalama Mkoa wa Singida, alikamatwa na Maofisa wa Takukuru kwa kupokea Sh 20,000 ili amsamehe Ramadhani Shumbi kutolipa kibali cha kuuza nyama.

Mtuhumiwa alikana mashtaka hayo na Hakimu, Nindi aliahirisha kesi hiyo hadi Juni 16 mwaka huu ambapo kesi hiyo itaanza kusikiliza hoja za awali. Mtuhumiwa yuko nje kwa dhamana ya Sh 1,000,000.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles