27.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

Ofisa Forodha kizimbani akidaiwa kukusanya Sh bil 1.8 bila utaratibu

NA KULWA MZEE-DAR ES SALAAM

OFISA Forodha wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Humphrey Lauwo, amefikishwa mahakamani kwa tuhuma za  kukusanya zaidi ya Sh bilioni 1.8 za kodi bila kufuata utaratibu. 

Mshtakiwa alifikishwa Mahakama ya Hàkimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam jana,

Mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Huruma Shahidi na kusomewa mashtaka na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon.

Akisoma mashtaka, Wankyo alidai kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo Julai 2, mwaka huu Dar es Salaam akiwa kama ofisa forodha mwandamizi wa TRA ambapo alikusanya Sh 1,803,323,055 bila kuruhusiwa na mamlaka hiyo. 

Ilidaiwa alikusanya fedha hizo ambazo zilitakiwa zilipwe kama kodi na Kampuni ya Puma Energy Tanzania Limited. 

Mshtakiwa alikana kutenda kosa hilo na upande wa mashtaka ulidai upelelezi wa kesi haujakamilika. 

Alirudishwa rumande baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana ambayo ni kuwa na wadhamini wawili wenye vitambulisho, watakaosaini dhamana ya maandishi ya Sh milioni 40 kila mmoja.

Kesi hiyo iliahirishwa hadi Septemba 9 kwa ajili ya kutajwa. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles