32.2 C
Dar es Salaam
Thursday, February 2, 2023

Contact us: [email protected]

Odom wa Khloe haambiliki kwa pombe

khloe-kardashianNEW YORK, MAREKANI

MWANAMITINDO maarufu nchini Marekani, Khloe Kardashian, anamtaka mpenzi wake, Lamar Odom, aache pombe.

Odom, ambaye alikuwa nyota wa kikapu katika Ligi ya NBA nchini Marekani, amekuwa mtumiaji wa pombe na dawa za kulevya na kumsababishia kulazwa hospitalini mara kwa mara.

Hata hivyo, madaktari wamemtaka nyota huyo aachane na dawa hizo pamoja na pombe, lakini kwa mara ya kwanza juzi alionekana akiwa anakunywa tena pombe alizokatazwa kunywa.

“Alikuwa na hali mbaya kutokana na matumizi yake ya pombe, madaktari walimtaka aache vitu hivyo, lakini naona bado, nimeamua kuingilia kati kumtaka aache kabisa pombe maana zitamletea matatizo.

“Ninaamini atanielewa kwa kuwa ananipenda na ninampenda, lakini kama atashindwa kunisikiliza mimi nadhani hakuna mtu atakayeweza kumsikiliza,” alisema Khloe.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,471FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles