29.3 C
Dar es Salaam
Thursday, June 1, 2023

Contact us: [email protected]

OCP Afrika yazindua mafunzo ya Kilimo chenye tija Kalambo

Na Jeremia Ernest, Dar es Salaam

Mkuu wa Wilaya ya Kalambo mkoa wa Rukwa, Kalolius Misungwi, amezindua mafunzo ya kilimo chenye tija yanayotolewa na kampuni ya OCP Afrika msimu wa pili Sumbawanga mjini.

OCP Afrika kupitia kampuni tanzu ya OCP Tanzania ilizindua awamu ya kwanza mradi wa tathimini ya udongo mwaka 2019 na awamu hii ya pili ya mradi huo unatarajiwa kuhudumia wakulima na wadau wa kilimo wa mikoa ya Rukwa, Morogoro, Mbeya na Iringa kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo, Idara za Kilimo (taasisi ya utafiti wa kilimo (TARI) kituo cha Uyole), tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI).

Mradi wa OCP SCHOOL LAB utatoa ushauri sahihi kwa mkulima mmoja mmoja na mapendekezo yanayolenga kuongeza tija ya mazao kama mahindi, mpunga, viazi pamoja na alizeti.

Akizungumza leo Mei 23, 2021 wakati wa uzinduzi huo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Joseph Mkirikiti, Mkuu wa wilaya ya Kalambo, Kalolius Misugwi amesema, sekta ya kilimo imeajiri asilimia 65 ya Watanzania wote.

“Sekta ya kilimo nchini imetoa ajira kwa kiasi kikubwa pia imelihakikishia taifa upatikanaji wa chakula kwa asilimia 100 pamoja na malighafi za viwandani, lakini bado idadi hiyo ya watanzania wanao jishughulisha na kilimo haipo katika uwiano sawa na idadi ya watanzania wote kwa sababu ya tija ndogo inayotokana na uzalishaji mazao, mpango huu utasaidia kuongeza na tija na bila shaka kuongeza uzaishaji wa mazao ya kilimo,” anasema Misungwi.

Kwa upande wa Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya OCP Tanzania, Dk. Mshindo Msolla amesema, kampuni hiyo ikishirikiana na Serikali imeandaa mchakato wa upimaji wa udongo kwa zaidi ya vijiji 100 ndani ya mkoa wa Rukwa.

“Lengo ni kuwaelimisha wakulima juu ya udongo wa eneo lao bila gharama zozote kwa wakulima hao majibu yatatolewa kwao pamoja na ushauri wa kitaalamu juu ya nini kifanyike ili kutunza ubora wa udongo wa kijiji husika kwa matokeo bora ya shughuli za kilimo, katika kila kijiji zaidi ya wakulima 100 watafikiwa na kuelimishwa namna bora za kufanya kilimo kiwe cha mahindi, mpunga au alizeti kulingana na maeneo waliopo,” amesema Dk. Msolla.

Ameongeza kuwa kwa mradi huu una tazamia kufikia wakulima 10,000 kwa mkoa wa Rukwa pekee kwakipindi cha mwaka huu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,225FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles