28.2 C
Dar es Salaam
Thursday, June 1, 2023

Contact us: [email protected]

Obi Mikel aivulia kofia Burundi

ALEXANDRIA, MISRI

NAHODHA wa timu ya taifa Nigeria, John Obi Mikel, ameimwagia sifa Burundi kwa kiwango walichokionesha katika mchezo wao wa ufunguzi kwenye michuano ya Afcon nchini Misri, juzi.

Nigeria walishuka dimbani dhidi ya wapinzani hao na kufanikiwa kushinda bao 1-0, Nigeria walipewa nafasi kubwa ya kushinda mabao zaidi ya moja, lakini mchezo ulionekana kuwa mgumu japokuwa walipata bao hilo.

Kikosi cha Burundi kikiwa chini ya kocha wao Olivier Niyungeko, kilionesha soka la ushindani wa hali ya juu na kuwashangaza wengi ikiwa ni mara yao ya kwanza kushiriki michuano hiyo mikubwa barani Afrika.

Kutokana na ugumu wa mchezo huo, Obi anaamini bado wana kazi ngumu ya kufanya katika kundi lao huku wakiziofia timu zingine kama vile Guinea na Madagascar.

“Ni kweli, sasa nimeamini kundi letu sio rahisi ni miongoni mwa makundi magumu sana, unaweza kuona ugumu wa mchezo wetu ulivyokuwa, Burundi walionekana kuwa timu ambayo ina umoja na imejipanga.

“Ilikuwa ngumu kupita katika safu yao ya ulinzi, lakini naweza kusema tulikuwa na bahati ya kupata ushindi huo, hata hivyo ndhani tulicheza vizuri na ndio maana tukafanikiwa kuondoka na pointi tatu,” alisema nahodha huyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,225FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles