27 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

OBAMA: NITAKUWA MWIBA KWA UTAWALA WA TRUMP

LIMA, PERU


Obama Discusses US Counterterrorism Policy At National Defense University

RAIS wa Marekani anayeondoka madarakani, Barack Obama, amesema hatakaa kimya iwapo mrithi wake, Donald Trump, atatishia maadili muhimu ya taifa hilo.

Msimamo huo wa Obama ni kinyume na utamaduni wa siasa za Marekani, ambao marais wa zamani huwa hawajiingizi katika siasa baada ya kuondoka madarakani na hawazungumzi kuhusu warithi wao.

Akizungumza katika kikao na wanahabari wakati wa Mkutano wa Nchi za Asia na Pasifiki (Apec) mjini hapa, Obama alisema anakusudia kumsaidia Trump na kumpa muda wa kueleza maono yake.

Lakini alisema kama raia, huenda akawa mwiba kwa kuzungumza kuhusu baadhi ya mambo atakayoona hayako sawa.

“Ninataka kuiheshimu ofisi na kumpa rais mteule fursa ya kueleza msimamo wake na mipango yake bila mtu kujitokeza kumkosoa,” alisema Obama.

Lakini akaongeza: “Iwapo suala litagusa maadili muhimu ya Marekani na imani yetu, nafikiri itabidi nitetee maadili hayo, nitalitathmini hilo wakati huo.”

Obama amesisitiza kuwa atatoa ushirikiano wa kutosha kwa kundi la Trump wakati huu wa mpito kama ilivyofanyika kwa kundi lake wakati wa kuondoka kwa mtangulizi wake George W. Bush.

Bush, tangu aondoke madarakani, amejizuia kuzungumzia utawala wa Obama.

“Sidhani hilo linasaidia kwa vyovyote. Ni kazi ngumu. Ana mambo mengi ya kushughulikia kwenye ajenda yake. Rais wa zamani hapaswi kuyafanya mambo kuwa magumu zaidi kwake.

“Marais wengine wa zamani wamechukua uamuzi tofauti; huu ni wangu,” Bush aliwahi kuliambia Shirika la Habari la CNN mwaka 2013 wakati Obama alipochaguliwa mara ya pili.

Msimamo wa Bush unafuata desturi, kwamba marais wa Marekani huwa wanajiepusha kuwakosoa watangulizi au warithi wao.

Lakini ufafanuzi wa Obama umekuja huku wasiwasi ukiendelea miongoni mwa makundi ya haki za kiraia kuhusu watu wanaoteuliwa na Trump kushikilia nyadhifa kuu katika Serikali yake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles