OBAMA ATAKA KOREA KASKAZINI ISHINIKIZWE

0
547

TOKYO, JAPAN


RAIS wa zamani wa Marekani Barack Obama amezitaka China na Korea Kusini kuendelea kuishinikiza Korea Kaskazini iachane na mpango wake wa silaha za nyuklia.

Alisema kwamba hiyo vikwazo vya biashara vinavyopunguza uwezekano wa kuishawishi kirahisi.

Obama amesema Korea ya Kaskazini ni mfano wa nchi ambayo iko mbali na kanuni za kimataifa yaani imetegwa na ulimwengu wote.

Rais huyo wa zamani wa Marekani aliyasema hayo kwenye ukumbi uliojaa mjini hapa jana katika hafla iliyoandaliwa na kundi la mashirika yasiyo ya kiserikali yanayosisitiza kuendelea kwa jitihada za kuifanya Korea Kaskazini iachane na mpango wake wa nyuklia.

Obama amezitaka China, Korea ya Kusini na Japan zinapaswa kuzidisha shinikizo kwa taifa hilo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here