29.2 C
Dar es Salaam
Monday, March 20, 2023

Contact us: [email protected]

Obama ampa ushauri Lionel Messi

US, MAREKANI

RAIS wa zamani wa Marekani, Barack Obama, ametoa ushauri wa bure kwa nyota wa timu ya taifa ya Argentina, Lionel Messi na wachezaji wenzake baada ya kushindwa kufanya vizuri katika Kombe la Dunia na Copa America.

Mwaka 2014, Messi alifanikiwa kuipeleka timu hiyo fainali kwenye Kombe la Dunia nchini Brazil, lakini hakuweza kutamba mbele ya Ujerumani mjini Rio de Janeiro, huku mwaka jana haikufanya vizuri kwenye michuano hiyo na walikuja kutolewa na Ufaransa ambao walikuwa mabingwa.

Obama alitaja sababu ambazo zinawafanya Argentina washindwe kufanya vizuri kwenye michuano mikubwa katika kipindi cha miaka ya hivi karibuni baada ya kufanya mahojiano na EXMA huko mjini Bogota nchini Colombia.

Obama alikuwa rais wa Marekani tangu mwaka 2009 hadi 2017, baada ya kumaliza kipindi chake nafasi yake ikachukuliwa na Donald Trump ambayo ndio rais wa sasa.

“Hata kwa watu ambao tunajua kwamba wana akili sana, lazima wafanye kazi kwa kushirikiana na wengine ili  kuwapa ujuzi. Timu ya Argentina ina Lionel Messi ambaye ana kiwango cha hali ya juu katika ulimwengu wa soka lakini inashindwa kufanya vizuri kwenye Kombe la Dunia.

“Ushauri wangu ni kwamba, wachezaji wenye umri mdogo wanatakiwa kutambua uwepo wa wachezaji wenye uwezo mkubwa ili kushirikiana vizuri kwa ajili ya kufanya vizuri,” alisema Obama.

Kauli hiyo aliitoa ikiwa ni siku chache kabla ya kuanza kwa michuano ya Kombe la Copa America mwezi ujao huko nchini Brazil, ambapo Argentina wamepangwa Kundi B, sambamba na Colombia, Paraguay na wageni waalikwa Qatar.

Argentina wanatarajia kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Nicaragua huko San Juan, Juni 7, kabla ya kupanda ndege kuelekea Brazil kwa ajili ya Copa America. Hadi sasa Argentina haijafanikiwa kutwaa taji kubwa tangu mwaka 1993, japokuwa ndani yake kuna Messi ambaye ni mchezaji bora duniani akiwa amechukua tuzo ya Ballon d’Or mara tano sawa na Cristiano Ronaldo.

Messi ametajwa kwenye kikosi cha Argentina pamoja na wachezaji wengine kama vile Sergio Aguero, Nicolas Otamendi, Roberto Pereyra na Juan Foyth.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
210,784FollowersFollow
563,000SubscribersSubscribe

Latest Articles