23.3 C
Dar es Salaam
Sunday, October 6, 2024

Contact us: [email protected]

Nyundo na wenzake wafungwa jela maisha

Na Mwandishi Wetu

Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma, imewahukumu kifungo cha maisha jela na faini ya sh 1 milioni kila mmoja washtakiwa wanne wa shauri la ubakaji na ulawiti wa Binti wa Yombo.

Washtakiwa hao katika kesi hiyo ya jinai namba 23476 ya mwaka 2024 ni aliyekuwa askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) MT 140105 Clinton Damas maarufu Nyundo, Amini Lema maarufu Kindamba, Nickson Jackson maarufu Machuche na Askari wa Jeshi la Magereza C 1693 Praygod Mushi

Kwa mara ya kwanza washtakiwa hao walifikishwa mahakamani August 19, 2024 na kusomewa mashtaka mawili ya kubaka kwa kundi na kumwingilia kinyume cha maumbile binti huyo ambaye Mahakamani anatambulika kwa jina la XY ambapo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Zabibu Mpangule Washtakiwa hao baada ya kusomewa mashataka walikana na kutokana na unyeti wa kesi hiyo hawakupatiwa dhamana ambapo baada ya kesi kusikilizwa kwa siku kadhaa leo wamesomewa hukumu na kukutwa na hatia hivyo kuhukumiwa kifungo cha maisha.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles