25.7 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 20, 2024

Contact us: [email protected]

Nyumba 5,000 kubomolewa Dar es salaam

bomoaRuth Mnkeni na Elizabeth Nyambele, Dar es Salaam

WIZARA ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imepanga kubomoa nyumba zaidi ya 5,000 za wakazi wa Jiji wa Dar es Salaam zilizojengwa kinyume na utaratibu na zilizo katika maeneo hatarishi.

Mpango wa kubomoa nyumba hizo ulitangazwa jana na mwanasheria wa Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Manchare Suguta, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika Bonge la Mkwajuni ambako jana shughuli ya ubomoaji ilikuwa ikiendelea.

Suguti alisema kazi ya ubomoaji wa nyumba hizo inafanywa kwa pamoja na Wizara ya Ardhi, Nyumba, Maendeleo na Makazi, NEMC na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam.

Alisema bomoabomoa hiyo itazihusu nyumba zilizojengwa pembezoni mwa bahari, maeneo yaliyo kwenye mabonde ya mito, wavamizi wa maeneo ya wazi na ambayo siyo rasmi kwa ujenzi.

“Hadi leo (jana) zaidi ya nyumba 260 tayari zimeshabomolewa na tunaendelea na kazi ya ubomoaji. Katika Bonde la Mto Msimbazi tunatarajia kufanya kazi ya kubomoa kwa siku nne na baada ya hapo tutahamia maeneo mengine,” alisema.

Suguti alisema Sheria ya mazingira ya mwaka 2004 kifungu cha 57 inazuia ujenzi wa nyumba za kuishi kwenye maeneo ya mito na vyanzo vya maji na iwapo kunakuwa na nyumba za makazi ya watu na shughuli zote za binadamu basi zijengwe umbali wa mita 60.

Alisema kazi ya Serikali ni kusimamia mali za wananchi na usalama wao hivyo kuwaondoa kwenye maeneo hatarishi ni hatua sahihi.

Aliyataja maeneo mengine ambayo ni hatari kwa makazi ya watu yanayokumbwa na bomoabomoa hiyo kuwa ni Mto Mlalakuwa, Mto Mbezi, Kawe, Gongolamboto na maeneo mengine.

Hata hivyo, wananchi waliobomolewa nyumba zao wamelalamika kuwa hawakupewa muda wa kutosha wa kuondoa vitu vyao na kutafuta sehemu nyingine ya kwenda kuishi.

“Jamani kwa kweli hata kama tumekosea lakini hii sio, tunafanywa kama wakimbizi watu mnakuja na bunduki kweli utadhani sisi sio Watanzania,” alisema Juma Mohamedi aliyejitambulisha kuwa ni mjumbe wa shina.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles