23.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

NYUMA YA PAZIA ‘KABLA YA KIKAO’ CHA MARAIS WA KOREA KASKAZINI, KUSINI


MWANDISHI WETU, MITANDAONI    |       

KATIKA picha ya pamoja wakati wakionana ana kwa ana kwa mara ya kwanza viongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-Un (alisimama upande kushoto) na Rais wa Korea Kusini Moon Jae-In (alisimama upande wa kulia). Itakumbukwa kuwa upande wa kushoto wa Kim Jong Un alikuwa amesimama katika ardhi ya Korea Kaskazini na Moon alisimama katika ardhi ya Korea Kusini. Katikati palikuwa na mpaka unaotenganisha nchi zao.

Baada ya salamu hiyo, Kim Jong Un alivuka kumfuata Moon Jae-In upande wa pili na kusalimiana tena, ikiwa ni ishara ya kuingia katika ardhi ya Jamhuri ya Korea Kusini.

Baadaye Kim Jong Un alirudi kwenye eneo lake, ndipo Moon akavuka kumfuata na kusalimiana tena ikiwa ni ishara ya kuingia ardhi ya Korea Kaskazini. Walisalimiana katikati. Wakasalimiana upande wa Korea Kusini. Wakahamia kusalimia pia upande wa Korea Kaskazini. Ilikuwa ishara ya ya kuvunja vunja minyororo ya uhasama uliodumu kwa miaka 65.

Lilikuwa jambo la kusisimua na la kihistoria. Dunia mzima imevutiwa kwa kufikia hatua hiyo ya makubaliano ya amani kati ya ndugu wa damu waliotenganishwa na falsafa.

Hata hivyo kukutana kati ya Kim Jong Un na Moon Jae In kumeanzia mbali. Tangu alipoingia madarakani mwaka 2011 Kim Jong Un alionekana mtawala shupavu na mwenye kiburi. Alifanya kila jaribio la kombora la nyukilia alilotaka. Sasa anaelekea kuachana na mpango huo baada ya mazungumzo yake na ‘ndugu’ zake Korea Kusini.

Mwanzo wa Xi Jinping

Machi 25, mwaka huu Kim Jong Un alisafari kwa treni hadi nchini China kukutana na Rais wa nchi hiyo Xi Jinping. Ziara ya Kim imetajwa kuwa ya siri. Baada ya uvumi wa siku nyingi, ilithibitishwa kwamba kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un amezuru China.

Ziara hiyo, ambayo ilithibitishwa na Serikali za China na Korea Kaskazini, ndiyo ya kwanza inayofahamika ya Kim nje ya Taifa lake. Kim alifanya mazungumzo ya kufana na Rais Xi Jinping mjini Beijing, ikiwa ni kabla ya mwezi mmoja baadaye kukutana na mwenzake Rais wa Korea Kusini, Moon Jae In mwezi uliopita.

Taarifa zinasema kuwa China ni mshirika mkuu wa Korea Kaskazini kiuchumi. Lakini mikutano miwili mizito ambayo alikabiliwa nayo Kim Jong Un, halijawa jambo la ajabu kukutana kwanza na kiongozi wa China. Wengi walitarajia kama ingetokea, lakini hawakujua nini kitazungumzwa kwenye mkutano na lini ungefanyika.

Ziara ya Beijing ilitazamwa na wengi kama hatua muhimu katika maandalizi ya Korea Kaskazini kuhusu mazungumzo yake ya kwanza na Korea Kusini na baadaye Marekani.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la China, Xinhua, wakati wa ziara hiyo, Kim Jong Un alimhakikishia Xi Jinping kwamba amejitolea kuacha kutengeneza silaha za nyukilia.

“Suala la kumalizwa kwa silaha za nyukilia kwa Rais wa Korea linaweza kutatuliwa, lakini iwapo tu Korea Kusini na Marekani watajibu juhudi zetu kwa nia njema, kuunda mazingira ya amani na uthabiti na pia kwa kuchukua hatua za kusonga mbele kwa pamoja kutoka kwa wadau wote kuhakikisha amani inapatikana,” Kim Jong Un alikaririwa akisema.

Kwa upande wake Shirika la Habari la Korea Kaskazini, KCNA, lilieleza ziara hiyo ilikuwa na umuhimu mkubwa katika kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hiyo na China.

“Inamaana kubwa kwa Korea Kaskazini kufafanua msimamo wake na kushirikiana na China, mshirika wake muhimu zaidi. Uhusiano huo umekuwa ulidhoofika katika miaka mitano iliyopita lakini haukufikia hatua ya hatari,” alisema Andray Abrahamian wa Taasisi ya Jukwaa la Pacific (CSIS).

Ziara ya Kim Jong Un nchini China ilifurahiwa na Serikali ya Marekani, ikiwa ni msururu wa shughuli nyingi za kidiplomasia tangu Korea Kaskazini na Kusini zilipoanza kuimarisha uhusiano wao wakati wa Michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi iliyoandaliwa Korea Kusini. China iliwasiliana na utawala wa Rais wa Marekani Donald Trump, na kuwafahamisha yaliyotokea katika mkutano huo.

“Tunatazama hili kama ishara nyingine kwamba kampeni yetu ya kuweka shinikizo kali ndiyo inayozaa matunda na kufanikisha mazingira mwafaka ya mazungumzo na Korea Kaskazini,” alisema msemaji wa Ikulu ya White House, Sarah Huckabee Sanders.

Yang Xiyu, mmoja wa waratibu wa mkutano wa China na Korea Kaskazini alisema, Kim Jong Un yuko wazi katika ukarabati wa mahusiano ya nchi yake na China. Amesisitiza kuwa kiutamaduni China na Korea Kaskazini ni marafiki wenye manufaa kwa miaka mingi hivyo basi kufungua mwelekeo mpya na Korea Kusini ni kubadili mchezo wa kidiplomasia na amani.

Xiyu ametaja maeneo yanayozingatiwa na Kim kuwa ni; kwanza kusitisha utengenezaji wa silaha za nyukilia , lakini kwa masharti. Pili, kupokea na kufanyia kazi ushauri wa Xi Jinping kama mshirika wake wa karibu. Tatu, Xi Jinping kutembelea Korea kaskazini kama sehemu ya kuimaraisha diplomasia baina ya nchi hizo. Mwisho ni kuzungumza na Marekani.

Safari ya siri ya Mike Pompeo

Aprili 18, mwaka huu Mkurugenzi wa Shirika la Upelelezi la Marekani, Mike Pompeo alisemekana kusafiri kwenda nchini Korea Kaskazini na kufanya mazungumzo ya siri na kiongozi wa nchi hiyo Kim Jong-un.

Vyombo vya habari vya Marekani viliripoti kuwa mkutano huo ni maandalizi ya mazungumzo ya ana kwa ana kati ya Rais Trump na Kim unaotarajiwa kufanyika Juni mwaka huu.

Trump anatajwa kuweka wazi kuhusu kufanyika kwa mazungumzo hayo ya moja kwa moja na kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un. Inaelezwa kuwa mazungumzo hayo ambayo hayakutarajiwa yataweka alama nyingine kama ya mwaka 2000 wakati Uongozi wa Juu wa Marekani ulipowasiliana moja kwa moja na Korea Kaskazini.

“Tulishawahi kuwa na mazungumzo ya moja kwa moja…katika ngazi za juu zaidi,” alisema Trump wakati wa ziara yake mjini Florida, alipokuwa akimkaribisha Waziri mkuu wa Japan,  Shinzo Abe.

Rais huyo alisema, ameshatoa ruhusa katika mazungumzo ya kujadili mkataba wa Amani ulioafikiwa wakati wa kumaliza rasmi vita ya Rasi ya Korea mwaka 1950 – 1953.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles