24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

NYOTA YA SIMBU YAZIDI KUNGA’RA

Na JENNIFER ULLEMBO-DAR ES SALAAM


ALPHONCE Simbu ametimiza ahadi aliyoweka kufanya vyema katika mbio ndefu za London Marathon zilizofanyika jana jijini London, England.

Akiwa Mtanzania pekee kwenye mbio hizo, Simbu alitumia muda wa saa mbili, dakika tisa na sekunde 10 kumaliza katika nafasi ya tano kwenye mbio hizo ambazo Mkenya, Daniel Wanjiru aliibuka mshindi.

Simbu ni miongoni mwa wanariadha wanaofanya vema hivi sasa katika mashindano ya kimataifa.

Mbali na kuipeperusha bendera ya Tanzania, mwanariadha huyo ameandika historia mpya katika mchezo wa riadha.

Ili kuhakikisha anatimiza malengo ya kuleta medali ya dhahabu nyumbani, Simbu ameweza kujifua kwa kuweka kambi za muda mrefu ndani na nje ya Tanzania.

Mashindano aliyoshiriki

I. All African Games mjini Maputo, nchini Msumbiji mwaka 2011, alipata nafasi hiyo baada ya kuchaguliwa na kufanya vema katika mashindano ya taifa kupitia mbio za mita 10,000.

II. Mwaka 2012-2013 alifanya majaribio na kushiriki mashindano mbalimbali ndani na nje ya nchi.

III. Mwaka 2014 alichaguliwa kujiunga na timu ya taifa kwa ajili ya mashindano ya Jumuiya ya Madola yaliyofanyika nchini Scotland.

IV. Mwaka 2015 alishiriki mashindano ya dunia ya Mbio za Nyika nchini China, pia aliweza kushiriki mashindano mengine na kufanikiwa kushika nafasi ya sita, ambapo alijikatia tiketi ya kushiriki mbio za Marathon Gold Cost kwa mara ya kwanza.

Simbu alifuzu na kupata nafasi nyingine ya kushiriki mbio za dunia zinazoandaliwa na Chama cha Wanariadha Duniani (IAAF) nchini China, alifanikiwa kumaliza katika nafasi ya 12 na kuchaguliwa kushiriki michuano ya Olimpiki Games iliyofanyika mwaka jana nchini Brazil.

V. Mwaka 2016 alialikwa katika mashindano yaliyojulikana kama Lake Biwa Marathon nchini Japan na aliweza kumaliza katika nafasi tatu za juu.

Mara baada ya kufanya vema kwenye mbio hizo, aliweza kuelekea Brazil katika michuano ya Olimpiki na kuweka rekodi nzuri kwa kumaliza nafasi ya tano.

VI. Simbu akiwa na ndoto kubwa ya kushinda medali ya dhahabu, kwa kudhihirisha hilo aliweza kuibuka bingwa wa mbio za Standard Chartered zilizofanyika nchini India mapema mwaka huu.

Mashindano yajayo

Mwanariadha huyo anakabiliwa na Mbio za Dunia za IAAF ambazo zimepangwa kufanyika Agosti 23, mwaka huu nchini Uingereza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles