23.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 28, 2021

Nyota Stars kurejea Blackpool

 ZAINAB IDDY – DAR ES SALAAM 

MCHEZAJI wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Adi Yussuf, ameweka wazi kuwa anataraji kurejea katika kikosi cha Blackpool, mara baAda ya mkataba wake wake wa mkopo katika klabu ya Boreham Wood kumalizika. 

Adi anayecheza katika nafasi ya ushambuliji alisema, atarejea Blackpool kwani mabosi wake hao wameridhishwa na kiwango alichokionyesha Boreham. 

“Nimeambiwa baada ya janga la corona kumalizika natakiwa kurejea Blackpool, kwa sababu wameona nipo fiti kuwasaidia katika mashindano mbalimbali. 

“Awali nililetwa Boreham Wood, kwa sababu sikuwa fiti kiushindani hali iliyotokana na kuugua, nashukuru hivi sasa huku walikonileta kumeniimarisha zaidi na nipo tayari kwa mapambano,”alisema. 

Wakati huo huo, Adi alisema yeye pamoja na wachezaji wengine wa Blackpool wapo katika majadiliano na klabu yao hiyo ambayo inataka kumpunguziwa kila mmoja asilimia 25 ya mshahara wake wakati huu wa janga la corona. 

”Tuliulizwa kuhusu utayari wa kupunguziwa asilimia 25 ya mshahara ili ikasaidiae waathirika wa corona, wachezaji kwa pamoja tumefanya majadiliano na kukubaliana na hilo kwa sababu hili tatizo ni la kila mtu duniani,”alisema. 

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
158,460FollowersFollow
519,000SubscribersSubscribe

Latest Articles